Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Van Persie: Arsenal hawawezi kushinda taji kocha akiwa Arteta

RVP X Arteta Van Persie: Arsenal hawawezi kushinda taji kocha akiwa Arteta

Sun, 27 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Arsenal ikilikosa taji la EPL dakika za jioni msimu uliopita na kuonekana wamejipanga kulinyakua msimu huu.

Mchezaji wa zaamani wa Klabu ya Arsenal, Mholanzi Robin Van Persie ametoa kauli ambayo pengine itawachukiza mashabiki wa Klabu hiyo.

Van Persie anasema ni ngumu kwa Klabu ya Arsenal kushinda taji ikiwa na Mwalimu kama Mikel Arteta na wasahau jambo hilo.

Akizungumza Van Persie anasema

"Arsenal hawawezi kushinda Taji huku Arteta akiwa meneja wao, simchukii lakini kama wachambuzi tunahitaji kusema ukweli. Arsenal inahitaji meneja ambaye ameshinda mataji mengi na mwenye mawazo ya ushindi yaliyowekwa kwa wachezaji "

"Arsenal sio klabu ambayo makocha wajao wanaweza kwenda kujifunza kufundisha, Arsenal sasa inahitaji meneja ambaye ameshinda mataji mengi na anataka kushinda zaidi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live