Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Van Nistelrooy ajitwisha mzigo wa Rashford

Rashford X Ten Hag Fresh Van Nistelrooy ajitwisha mzigo wa Rashford

Tue, 27 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ruud van Nistelrooy ameamua kujitwisha mzigo wa kuhakikisha anamfanya mshambuliaji Marcus Rashford anarudi kwenye ubora wake.

Rashford bado anapambana na hali yake kurudi kwenye ubora wake kwa miaka miwili sasa, wakati huko nyuma alikuwa mmoja wa wachezaji tishio sana kwenye kikosi cha Manchester United.

Na sasa Van Nistelrooy, ambaye amerejea Man United kuwa msaidizi wa kocha Erik ten Hag amekuwa na vipindi maalumu vya mazoezi na Rashford ili kuhakikisha anarudi na kuwa tena bora uwanjani.

Rashford, 26, hajafunga bao kwa muda mrefu sana kwenye kikosi hicho cha Man United. Msimu wake bora alishuhudiwa akifunga mabao 34 karibu miezi 20 iliyopita.

Na sasa Man United inaamini Van Nistelrooy – ambaye alifunga mabao 150 katika miaka yake mitano Old Trafford – ataweza kurudisha makali ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England.

Hivyo, Mdachi huyo amekuwa akimfua Rashford kwenye mazoezi maalumu ili kuhakikisha anakuwa bora tena. Fowadi huyo baada ya kushindwa kufunga kwenye mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England dhidi ya Fulham, alitoka tena kapa katika mechi ya pili dhidi ya Brighton, Jumamosi.

Rashford alitumbukiza mpira nyavuni kwenye mechi hiyo ya kichapo cha mabao 2-1, lakini bao lake lilikataliwa na VAR baada ya kuonekana aliotea.

Man United ilipoteza mechi hiyo baada ya kuruhusu bao katika dakika za majeruhi lililofungwa na Joao Pedro.

Chanzo: Mwanaspoti