Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Van Dijk amzungumzia Coady Gapko

Virgil Van Dijk Gakpo Van Dijk amzungumzia Coady Gapko

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa timu ya taifda ya Uholanzi Virgil Van Dijk amemzungumzia kinda wa timu hiyo Coady Gapko kuhusu kuhusishw na vilabu vikubwa duniani.

Kinda Coady Gapko mwenye umri wa miaka 19 ambae anaonekana kufanya vizuri kwa sasa baada ya kua na msimu mzuri na klabu yake ya Psv Eindnhoven na sasa akiwa nafanya vizuri na timu ya taifa ya Uholanzi kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar.

Kinda huyo ambaye alikua anakaribia kujiunga na klabu ya Manchester United mwishoni mwa dirisha la usajili lililopita kwenye majira ya joto. Lakini kwasasa imeonekana vilabu vingi kuvutiwa na mshambuliaji huyo kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha.

Van Dijk ameongelea kuhusu tetesi hizo kumhusu Gapko “Gapko kwenda Manchester United au Real Madrid, Manchester na Real Madrid jr zipo kiwango sawa kwasasa? Hakuna kutokuheshimu kabisa”

Van Dijk aliendelea kwa kusema “Gapko ni kijana mzuri, anapambana sana na mwenye kipaji kuna mengi yanakuja kutoka kwake” Beki huyo anaamini mchezaji huyo mwenye mabao matatu mpaka sasa kwenye kombe la dunia ana kipaji kikubwa na hakuna uvunjifu wa heshima yeye kuhusishwa na vilabu kama Real Madrid kwasababu ana kipaji kikubwa na uwezo wake pia unaonekana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live