Valencia imefungwa kwa sehemu ya uwanja katika mechi tano kufuatia zijazo kufuatia dhuluma ya kibaguzi aliyofanyiwa mshambuliaji wa Real Madrid Vinicius Jr.
Polisi wa Uhispania wamewazuilia watu watatu kuhusiana na unyanyasaji ulioelekezwa kwa Mbrazil huyo kwenye Uwanja wa Mestalla siku ya Jumapili.
Valencia pia wamepigwa faini ya euro 45,000 (£39,000).
Uwanja wa kusini wa Valencia utafungwa na klabu ina siku 10 kukata rufaa.
Shirikisho la Soka la Uhispania (RFEF) pia lilisema Vinicius, 22, hatasimamishwa baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 97 na yuko huru kucheza mechi ya Jumatano dhidi ya Real Vallecano.
RFEF ilisema katika taarifa yake kwamba uamuzi wa mwamuzi wa kumfukuza Vinicius ulitokana na yeye "kunyimwa sehemu muhimu ya ukweli", na kuongeza kuwa "haiwezekani kutathmini vizuri kile kilichotokea".
Mechi hiyo ilisitishwa katika kipindi cha pili huku Vinicius aliyekasirishwa akiwashitaki kwa mashabiki wa timu pinzani kwa mwamuzi.
Real imewasilisha kesi ya unyanyasaji dhidi ya Vinicius kwa ofisi ya mwendesha mashtaka wa Uhispania kama uhalifu wa chuki.