Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Valencia CF Wamtimua Rais wa Klabu

Rais Valencia Murphy Anil Murthy

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Valencia CF imethibitisha kumfukuza Rais wa klabu hiyo Anil Murthy baada ya kuvuja kwa jumbe ya sauti ambayo inasikika akimtisha mchezaji iwapo ataondoka hyuru na kumkosoa mmiliki wa klabu hiyo Peter Lim hivyo kuchafua sura ya Klabu.

Kwenye waraka wa klabu ya Valencia ulisema,

“kubadili uongozi kunahitaji kupata imani ya mashabiki na jamii kwa pamoja ili kuiweka Valencia CF kwenye nafasi nzuri ya mafanikio. Kwa hatua za haraka, Anil Murthy atakoma kuwa Rais na muajiriwa wa Valencia CF.”

Kwenye jumbe ya sauti iliyorekodiwa, na kuchapishwa April na gazeti Valencian newspaper Superdeporte, Murthy alisikika akimtishia kuaharibu heshima yake kiungo wa klabu ya Valencia Carlos Soler ikiwa tu ataondoka klabuni hapo huru.

Murthy alisikika tena kwenye jumbe iliyotenganishwa akimuita Lim “asiyejiweza” huku akidai kuwa mmiliki wa klabu hiyi ni mshabiki sana kufanya maamuzi muhimu kwa ajiri ya biashara.

“Bodi ya klabu hiyo imethibitisha kuwa maneno yaliyovuja ya mazungumzo kati ya Anil Murthy na aliokuwa akifanya nao mazungumzo ni maono yake yeye na sio ya Valencia CF. Valencia CF haihisiki na maono yake.” Waraka ulisomeka

Murthy kuondoka kwake kuna kunatengeneza sintofahamu ya nani atakayeweza kuchukua nafasi yake kwenye kipindi ambacho klabu ipo kwenye kipindi kigumu. Ambapo wachezaji wamekuwa wakipitia kipindi kigumu cha kupunguzwa mishara na wale wachezaji muhimu wakiuzwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live