Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uzoefu mdogo tatizo Ihefu- Katwila

C92633d205340a951d93f783258c3d96 Uzoefu mdogo tatizo Ihefu- Katwila

Fri, 23 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA wa timu ya Ihefu, Zuberi Katwila amesema kutokuwa na wachezaji wazoefu ni chanzo kwa kikosi hicho kufanya vibaya kwenye mechi za Ligi Kuu.

Ihefu ina pointi tatu ilizopata baada ya kucheza mechi saba imeshinda mchezo mmoja huku zingine zote ikiambulia kichapo hali inayoifanya kushika nafasi ya pili kutoka mkiani kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Katwila aliyekiongoza kikosi hicho kwenye mchezo mmoja uliopita waliofungwa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC, alisema amegundua uzoefu ni tatizo na sasa ameanza kuwajenga wachezaji hao kisaikolojia.

“Wachezaji wengi wanaounda kikosi ni chipukizi hawana uzoefu na mechi za ligi ndio maana imekuwa changamoto kupata ushindi nimegundua sasa nawajenga kisaikolojia kuwajenga upya,”alisema Katwila.

Alisema atatumia mbinu na uzoefu alioupata kwenye timu yake ya zamani Mtibwa Sugar ambayo kwa muda mrefu ilikuwa na utamaduni wa kuwapandisha wachezaji chipukizi kwenye kikosi.

Katwila amejiunga na kikosi hicho baada ya kutangaza kujiuzulu kuinoa timu ya Mtibwa Sugar aliyoifundisha kwa karibu misimu mitatu kwenye ligi hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz