Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uzoamaka Confidence Igwe, mashine ya kazi Jangwani

Igwe Fc Uzoamaka Confidence Igwe

Tue, 10 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MFAHAMU MCHEZAJI HUYU MPYA WA YANGA PRINCESS.

Leo nipo kwa kitasa, akili mingi nguvu kidogo kama Bacca tu.

▶ Majina yake kamili: Uzoamaka Confidence Igwe.

▶ Amezaliwa tarehe 15/5/1997 (27yrs).

▶ Raia wa Nigeria.

▶ Mguu anaoutumia zaidi uwanjani: Kushoto.

▶ Nafasi uwanjani : Beki wa kati (CB) ndio nafasi anayotumika zaidi,, Pia anamudu kucheza kama beki wa kushoto (LB),Kiungo wa ukabaji (DM), kiungo mshambuliaji (AM) na Mshambuliaji wa kati (CF).

⏩ Amesajiliwa na Yanga Princess akitokea Wadi Degla Ya Misri.

⏩ Mchezaji aliyeweka alama kubwa kwa mashabiki wa klabu ya Bayelsa Queens ya kwao Nigeria, akiitumikia kwa miaka 10 huku akiwa nahodha wa kikosi.

Jina lake limewekwa kumbukumbu kwenye klabu hiyo kwa utumishi wake bora akiwa hapo.

Kuna kichekesho kiliwahi kutokea mwaka 2021 Beki huyu aliuzwa kwenda kwenye klabu ya Malabo Kings FC Women ya Equatorial Guinea kwa dau kubwa ambalo viongozi wa Bayelsa Queens waliona faida kwa timu, lakini mashabiki wa timu hiyo walichanga pesa na kuvunja mkataba akiwa ameitumikia miezi 6 pekee timu yake mpya, akarudishwa Bayelsa Queens.

Ndipo baadae aliruhusiwa kuondoka kwenda Misri kwa kuagwa rasmi kama legendary wa timu,huku akitajwa kuwa ni darasa kwa watoto wengi wa kike wenye ndoto za kucheza soka kutokana na nidhamu yake na kipawa cha uongozi alichonacho pamoja na kujituma kwake.

⏩ Igwe awapo uwanjani tegemea kuona haya

..Utulivu wa hali ya juu

..Kiongozi mahiri uwanjani kwa maneno na vitendo.

..Uwezo wa kuzuia mashambulizi.

⏩ Uzoamaka Igwe ni beki ambaye anatumia akili kwenye uzuiaji tunaita Defending Control Style ,Uzuiaji ambao unategemea zaidi ball control,habutui hovyo,anatunza mali anakulaza huyoo mbele kaenda.

⏩ Anaitumikia pia timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria,

⏩ Akiwa kwenye klabu ya Bayelsa Queens kama nahodha na kama beki amecheza pacha na beki mwingine aliyesajiliwa na Yanga Princess msimu huu ANGELA MICHAEL ambaye ndie aliyerithi kitambaa cha unahodha baada ya Igwe kutimukia Misri,Awamu hii wamekutana tena jangwani.

Pia nae anaitumikia timu ya taifa ya Nigeria kwa upandw wa wanawake.

⏩ Ukimuangalia waweza sema ni wakawaida sana ila huyu ni beki ya kazi.

Wananchi eneo la ulinzi kwa upande wa sisi dada zenu tumepata watu wa maana kabisa kuanzia kipa,mabeki wa kati mabeki wa pembeni aaah weeee huu mwaka watasema yote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live