Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uzembe waiponza Yanga, kukumbana na rungu la CAF

Yanga Caf Mks Uzembe waiponza Yanga, kukumbana na rungu la CAF

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga inaweza ikakumbana na rungu la Shirikisho la Soka Africa CAF kwa kushindwa kuvaa beji za CAF Champions League bila sababu ya msingi.

Kwenye mechi zake mbili za makundi ya Champions League dhidi ya CR BELOUZIDAD ugenini na ile ya Ahly nyumbani Yanga haikuwa na beji hizo kwenye jezi zake kama taratibu zinavyosema.

Kitendo hicho kinashawishi adhabu ya faini kutoka kwa mamlaka husika. Beji huwa zinapelekwa kwenye mashirikisho ya nchi ili vilabu shiriki vikachukue huko na kuzishonea kwenye jezi za mechi zao za mashindano ya vilabu barani Afrika.

Taarifa za uhakika kutoka chanzo cha ndani ya CAF zinasema beji zilifika TFF kwa wakati na TFF walifanya jitihada kuwasiliana na Simba na Yanga ambapo Simba walichukua beji zao na kuzitumia wakati Yanga hawakufanya hivyo bila taarifa yoyote.

Kwenye kikao cha mechi (Pre-match meeting/Technical meeting) kwenye mechi dhidi ya Ahly, kiongozi anaehusika kutoka klabuni inasemekana alikiambia kikao kwamba beji hazijafika ilihali zilikuwepo ila wao hawakwenda TFF kuzifata.

Chanzo cha kuaminika kinasema TFF kupitia maafisa wake walijitahidi kuwasiliana na Yanga mpaka siku ya mechi na Ahly kuhusu hizo beji bila mafanikio.

Taarifa kutoka Yanga zinasema viongozi hawajafurahishwa na uzembe uliofanywa na viongozi wahusika wa idara ya mashindano ya klabu kwa kushindwa kuchukua beji hizo TFF na sasa wamembadilisha mtu wa kusimamia masuala hayo ya mashindano baada ya tukio hili.

Bin Kazumari ilipokea meseji nyingi za wafuatiliaji wake wakitaka kufahamu kwanini Yanga hawavai beji za CAF kwenye jezi zao za CHAMPIONS LEAGUE, baada ya ufuatiliaji hayo ndo majibu.

BINA KZAUMARI (The voice of the voiceless)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: