Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja wakwamisha mechi Ligi Kuu

Uhuru Pic Uwanja wakwamisha mechi Ligi Kuu

Fri, 16 Sep 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Klabu ya Ruvu Shooting imetangaza kuahirishwa kwa mechi yake ya Ligi Kuu duru ya nne dhidi ya Polisi Tanzania iliyotarajiwa kupigwa leo Septemba 16,2022 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni huku Sababu kuu ikiwa ni dimba hilo kuwa na matumizi mengine.

Taarifa rasmi ya Ruvu Shooting imeeleza kuahirishwa kwa mchezo huo na kupangiwa tarehe nyingine (Septemba 16,2022) kutokana na uwanja wa Uhuru kuwa na matumizi mengine kwa siku ya leo.

Ruvu yenye masikani yake Mlandizi, Pwani kwa misimu kadhaa nyuma ilikuwa ikitumia uwanja wa Mlandizi kwenye mechi zake za nyumbani lakini msimu huu mambo yamebadilika baada ya dimba hilo kukosa sifa.

Hilo lilipelekea Ruvu kuchagua kutumia uwanja wa Uhuru kwenye mechi zake za nyumbani lakini hata hivyo haijacheza mchezo hata mmoja katika dimba hilo hadi sasa kwani mechi zote tatu ilizocheza ilikuwa ugenini.

Mechi hizo ni ile ya ufunguzi wa ligi dhidi ya Ihefu iliyopigwa Highland Estate, Mbeya na maafande hao kushinda 1-0, na mechi ya pili ikipoteza Manungu, Morogoro kwa kuchapwa 2-1 na Mtibwa Sugar huku mechi ya tatu ikifungwa 1-0 na Namungo kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Chanzo: Mwanaspoti