Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja wa Valencia uliotelekezwa kwa miaka 14, Umeua watu, una gundu

Uwanja Valencia Uwanja wa Valencia uliotelekezwa kwa miaka 14, Umeua watu, una gundu

Sun, 7 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Tangu msimu wa 2009-10, Valencia imekuwa na ndoto isiyotimia ya kuhamia kwenye uwanja wao mpya Nou Mestalla ambao ungeweza kuingiza mashabiki 80,000 na sasa miaka 14 imepita.

Stori ilianza mwaka 2007, wakati Valencia ilipokuwa na wachezaji vijana kama David Villa, Pablo Aimar, David Silva na Juan Mata waliokuwa na vipaji vikubwa. Wakati huu Valencia ilikuwa bora na ikatajwa kama moja ya timu ya tatu tishio nchini Hispania kutokana na makali yake.

Walikuwa wakifananisha na ukubwa wa Real Madrid na Barcelona na ili kuthibitisha hilo, mabosi wa Valencia wakaamua kuja na mpango wao wa kujenga uwanja mkubwa ambao ungeweza kuingiza mashabiki 80,000.

Uwanja huu ungekuwa moja ya viwanja 10 vya soka vikubwa Duniani na haikuchuku muda kazi ikaanza.

Lakini mambo yaliingiliana baada ya Valencia kupatwa na anguko kubwa la kiuchumi na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2008 wakawa na deni la Pauni 350 milioni. Hii ilisababisha ujenzi usimame.

Lakini ndoto ya kukamilisha ujenzi waliouanza ikawa pale pale na ili kufanikisha hilo ikauweka sokoni uwanja wao wanaoutumia sasa ili pesa ambazo wangepata ndio zitumike kwenye ujenzi lakini bahati mbaya hawakupata mnunuaji.

Mabosi wa Valencia hawakuishia hapo walijaribu hata kwenda kukopa Pauni 90 milioni lakini hakuna benki iliyokubali kuwakopesha, hivyo ujenzi wa uwanja wa ndoto yao ukasimama rasmi February 2009.

ULIVYOCHUKUA ROHO ZA WATU

Mei, 2008 wakati kazi ya kuujenga uwanja huu ilipokuwa inaendelea watu wawili walipoteza maisha baadaya vyuma kuwadondokea kutoka juu kwa urefu wa futi 25. Watu hao wawili ambao walikuwa ni wanaume hawakufa papo hapo bali ilichukua siku kadhaa tangu wakumbe na tukio hilo.

NINI KILITOKEA BAADA YA HAPO

Imepita miaka 14 sasa, tangu ujenzi wa uwanja huo usimame, na sasa Valencia imeendelea kucheza kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Mestalla wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 49,430.

Inaidaiwa kuwa Desemba 2011, Valencia ilifikia makubaliano na kampuni ya Bankia ili kampuni hiyo imalizie matengenezo ya uwanja huo mpya halafu malipo yao yangekuwa ni kuchukua uwanja unaotumiwa na Valencia kwa sasa lakini dili lilifeli kwenye dakika za mwisho.

Miaka miwili baada ya hapo Valencia iliingia kwenye mazungumzo na kampuni ya Fenwick Iribarren ili watengeneze uwanja huo.

Fenwick Iribarren ikatoa mapendekezo ya kupunguzwa kwa ukubwa wa uwanja ikiwa pamoja na siti za mashabiki kutoka 80,000 hadi 61,000, lakini hapa pia mchakato ulishindikana.

Kulikuwa na taarifa pia kwamba yaliwasilishwa maombi kwa Manispaa ya Valencia ili itoe pesa za kukamilisha uwanja huo mwaka 2017 na ukimalizika uwe una umiliki wa serikali na Valencia kwa asilimia lakini jambo likafeli pia.

Jambo la gundu la gundu tu, Juni mwaka jana Valencia yenyewe ilijaribu kuja na mpango mpya wa kutoa pesa kutoka kwenye mfuko wa timu na kutengeneza uwanja huo lakini taarifa zinadai ungetengezwa kwa udogo kuliko uwanja wao wa sasa.

Mpango huu ulikuwa umepitishwa ili uwanja uanze kutengenezwa Oktoba lakini hadi leo hakuna kinachoendelea.

Ukiuona kwa sasa umegubikwa na vumbi kwa sababu ya kuachwa muda mrefu na yamekuwa ni makazi ya ndege na wadudu wa aina mbali mbali.

Chanzo: Mwanaspoti