Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja wa Uhuru unahitaji haya

Uwanja Wa Uhuru Dar Uwanja wa Uhuru unahitaji haya

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Uwanja wa Uhuru uliopo Tamaeke jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa viwanja vikongwe nchini ambavyo nyuma yake vina historia ya kipekee katika seklta ya michezo, ukiondoa ukweli kwamba ndipo ambapo Tanganyika ilisherekea kupata uhuru wake zaidi ya miaka 62 iliyopita.

Ni katika uwanja huo pia timu mbalimbali zikiwamo kutoka mataifa yaliyoendelea za soka kama Uingereza na Brazil zilifika na kucheza na klabu za hapa nchini katika miaka ya zamani na kwa hiyo ni uwanja ambao una historia yake.

Pia ndio uwanja ambao pengine umeandaa mashindano mbalimbali ya ndani na kimataifa kwa wingi zaidi kuliko viwanja vingine ukiwa pia na rekodi kadhaa ambazo zimewahi kubeba furaha na huzuni za wanamichezo na timu zetu kwa nyakati tofauti katika miaka ya zamani.

Ni kwa sababu hiyo Uhuru unabaki kuwa uwanja pekee ambao una kila sababu ya kuenziwa na kufanywa kuwa eneo la kumbukumbu ya michezo na sekta zingine. Hata hivyo, lililo dhahiri ni kwamba kwa wanamichezo Uhuru ni kila kitu kwao.

Wakati uwanja huo ukiwa umefungwa kwa ajili ya ukarabati, uwanja huo wenye hadhi kubwa unapaswa kuwa na mwonekano mzuri ambao utaupa thamani kubwa na usiwe na kasoro kadhaa ambazo zitaathiri au kupoteza maana ya uwepo wake.

Maboresho ya kwanza ni ya eneo la kuchezea ambalo linaonekana halina ubora na nyasi bandia ambazo zipo zinaonyesha kuzeeka na kuchakaa, lakini pili ni miundombinu ya utoaji majitaka.

Uwanja huo unapaswa kuondolewaa kasoro katika vyoo ambako kumekuwa na hali isiyo nzuri kwa muda mrefu na kuwekewaa mandhari ambayo yatawafanya watumiaji wake kufurahi michezo na pia kufurahi wanapokwenda maliwatoni.

Pia kuna changamoto ya kutokuwepo na mazingira salama na tulivu kwa waandishi wa habari kutimiza majukumu kunapokuwa na mchezo ambapo mara kwa mara wamekuwa wakichanganywa na mashabiki, hivyo hupata wakati mgumu katika utendaji wa kazi.

Tunadhani ni vyema mabenchi ambayo yanatumiwa na wachezaji wa akiba nayo yakabadilishwa, kwani yaliyopo sasa yamepasuka na hivyo kuyakosesha mvuto na hata mvua inaponyesha maana yake wachezaji na maofisa wa benchi la ufundi hulowa.

Tanzania ni nchi inayotajwa kupewa sifa ya kuwa na mwamko mkubwa kisoka, jambo ambalo linaifanya ifuatiliwe kwa ukaribu na kundi kubwa la watu kila kukicha.

Hii imechangia kwa kiasi kikubwa kutoa ushawishi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuipa Tanzania uenyeji wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2027 ambapo itaandaa kwa pamoja na Kenya na Uganda na hivyo ubora wa viwanja kama Uhuru ndio utatoa ishara kuwa tupo tayari kuandaa fainali hizo na kinyume chake tutatengeneza mazingira ya kuwapa wengine wanaoonyesha utayari.

Hiyo inamaanisha kwamba tumeshakuwa wakubwa kwenye soka Afrika. Kuonekana kwa uwanja ambao una kasoro nyingi kunashusha thamani na hadhi ya nchi yetu, hasa katika kipindi hiki ambacho tunapambana kuinua sekta ya utalii.

Chanzo: Mwanaspoti