Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja wa Mkapa kufungwa skrini za kisasa za matangazo

Uwanja Wa Benjamin Mkapa Stadium Uwanja wa Mkapa kufungwa skrini za kisasa za matangazo

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imetangaza kuingia ubia na kampuni Mama ya kitanzania ya Formula360 Ltd katika uwekaji wa matangazo ya kidigitali katika uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa kwa lengo la kuongeza mapato kwa Serikali.

Formula360 Ltd ni kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikifanya shughuli za utangazaji wa kidigitali na usio wa kidigitali pamoja na kununua matangazo kutoka vyombo vingine vya habari.

Kupitia ushirikiano huo Formula360 itawekeza shilingi Bilioni moja katika ufungwaji wa TV (screen,) kuzunguka uwanja wa Taifa na kutoa nafasi kwa Wadau kutangaza matangazo mengi katika uwanja huo unaobeba mashabiki wapatao 60,000.

Kabla ya makubaliano haya uwanja wa Taifa ulikuwa ukitumia matangazo tuli yenye kiwango na ubora hafifu na ujio wa Formular360 utafanya matangazo hayo kuwa ya kisasa pamoja na kupendezesha uwanja.

Kampuni ya Formula360 Ltd inamilikiwa na kuendeshwa na Watanzania na inaendelea kufungua njia kwa kampuni za ndani kushiriki katika juhudi za kuleta Maendeleo ya Taifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live