Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja wa KMC upendwe na kutunzwa

GSCv YpWIAAEumd.jpeg Uwanja wa KMC upendwe na kutunzwa

Fri, 12 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imetimiza rasmi ahadi ya kuwa na uwanja wa soka ambao utatumiwa na timu inayoimiliki ya KMC inayoshiriki Ligi Kuu Bara.

Sio tu KMC tu, uwanja huo pia unaweza kutumiwa na timu nyingine tofauti pamoja na kutumika kwa matukio mbalimbali ya kimichezo na kijamii kwa ruhusa kutoka kwa wamiliki.

Mfano tunashuhudia hivi sasa ukitumika kwa mechi za mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) na mechi mbili za ufunguzi zilichezwa hapo, ya kwanza ikiwa ya Al Wadi ya Sudan dhidi ya JKU ya Zanzibar na baadaye Coastal Union ya hapa nyumbani ikaumana na Dekedaha ya Somalia na mechi za jana za kundi A.

Kuanza kutumika kwa Uwanja wa KMC pale Mwenge kuna faida kubwa kwa wamiliki ambao ni Manispaa ya Kinondoni pamoja na jamii ya watu wa soka kijumla.

Sidhani kama kunahitajika maelezo ya faida zinazoweza kupatikana kutokana na uwepo na kutumika kwa uwanja huo, kwani zinafahamika na wadau wa na hata wale ambao sio wapenzi wa soka.

Kutokana na hilo, ni jukumu na wajibu wetu kuupenda uwanja huo na kuuthamini jambo ambalo litasababisha kuutunza ili kuuepusha na uharibifu ambao utachangia kuufanya upoteze ubora na thamani yake.

Mtu anayekipenda kitu atajitahidi kukilinda kwa wivu mkubwa kwa vile kikiharibika kitampa maumivu moyoni mwake tofauti na yule ambaye hakipendi kwani hatoona maana ya uwepo wa kitu hicho.

Kila mmoja wetu anapaswa kuwa mlinzi wa mwenzake uwanjani hapo na kuhakikisha hatoi mwanya wa uharibifu au wizi wa kitu chochote jambo litakalouacha salama.

Chanzo: Mwanaspoti