Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja wa CCM Kambarage wafungiwa

Kambarage CCM.jpeg Uwanja wa CCM Kambarage wafungiwa

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya ligi kuu Tanzania (TPLB) imeufungia uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, kutumika kwa michezo ya ligi kuanzia jana Oktoba 3, 2023, Kwa kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.

Bodi ya ligi imesema kuwa, uwanja huo umekosa nyasi za kutosha katika eneo la kuchezea (Pitch) pamoja na kutokuwa na tambarare jambo linalosababisha mtiririko wa mpira kutokuwa sawa.

Sababu nyingine ni pamoja na kuwa na muonekano usiovutia kwa watazamaji wanaohudhuria uwanjani na wanaotazama michezo ya ligi kupitia runinga.

Bodi ya ligi imeitaka Klabu ya JKT Tanzania FC kuchagua na kutuma jina la uwanja mwingine itakaotumia kwa michezo yake ya nyumbani hadi pale uwanja wa CCM Kambarage utakapofanyiwa maboresho, kukaguliwa na kuthibitishwa kuwa unafaa kutumika kwa michezo ya ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live