Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja wa AFCON kuanza kujengwa Arusha

Uwanja Arusha 1.jpeg Uwanja wa AFCON kuanza kujengwa Arusha

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumamosi iliyopita, Novemba 18, 2023 Fainali za Chuga Cup 2023 zilihitimishwa katika Dimba la General tire ambapo ambapo Timu ya Kaloleni FC waliibuka mabingwa ambapo mgeni rasmi wa fainali hizo alikuwa Waziri wa utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Damas Ndumbaro.

Akizungumza mara baada mchezo huo kutamatika, Dr. Ndumbaro alisema Arusha imepata bahati ya kuwa miongoni mwa mikoa michache nchini ambayo uwanja wa Kimataifa kwa ajili ya michuano ya AFCON2027 utajengwa mkoani humo.

Ndumbaro amesema kuwa mpaka Januari mwaka, uwanja huo utakuwa umeanza kujengwa sambamba na viwanja vingine vitano vya mazoezi vyenye hadhi ya kimataifa ahuku akisisitiza kuwa msimu ujao watapeleka watalaam wa kutambua vipaji ‘scouting’ kwenye mashindano hayo ili kuwachukua vijana wenye vipaji na kuwapeleka timu kubwa.

Kwa upande wake, Mrisho gambo amesema kuwa mabingwa wa mchuano hiyo licha ya kupewa zawadi nono, watapelekwa pia Bungeni Dodoma na kwamba lengo lake ni kuboresha zaidi michuano hiyo msimu unaokuja ikiwa ni pamoja na kuongeza zawadi na idadi ya timu zitakazoshiriki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live