Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja mpya wa Madrid ni sawa na viwanja 16 vya Mkapa

Reforma Santiago Bernabeu Uwanja mpya wa Madrid ni sawa na viwanja 16 vya Mkapa

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

  Headline isikuvuruge sana hesabu zipo hivi, uwanja mpya wa Real Madrid ambao unafanyiwa marekebisho unaripotiwa kugharimu kiasi cha US Dollar Bilion 1 ambazo ni sawa na shilingi Trilioni 2.5 za kitanzania.   Ukija kwenye Uwanja wa Mkapa wenyewe kwa mujibu wa mitandao inaonyesha kuwa uligharimu US Dollar milioni 56 ambazo ni sawa na shilingi Bilioni 140.2 za kitanzania.   Sasa ukipiga mahesabu ya Bilioni 140 zilizotumika kujenga Uwanja wa Mkapa unapata jumla ya viwanja 16 kwenye Trilioni 2.5 zilizotumika kuujenga Uwanja mmoja wa Santiago Bernabeu.   Unaweza ukawaza ni kwa namna gani timu inaweza kujenga kiwanja cha gharama kiasi hiko kisha ukafikiria sisi kama taifa zima tunashindwaje kujenga hata viwanja vitano kama ule wa Taifa,tuachane na hayo.   Uwanja wa Bernabeu ukimalizika rasmi 2024 utakuwa uwanja wa pili kwa Uwanja uliotumia pesa nyingi zaidi Ulaya nyuma ya Wembley huku ukitarajia kushika nafasi ya 15 duniani.   Sababu kubwa ya Bernabeu kutumia pesa nyingi ni pamoja na kuwa na viwanja 6 ambavyo vimepangana kutoka chini ya ardhi.   Kwa maana uwanja huo una uwezo wa kubadilika eneo(pitch) la kuchezea baada kutumika katika mchezo husika,mfano wakicheza mechi ligi,wanaweza kubadilisha eneo(pitch) la kuchezea likashuka chini kisha wakaleta eneo(pitch) lingine la kuchezea,yapo maeneo (pitch) 6.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live