Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja kujaa barafu sababu mechi ya Burnley vs Tottenham kuahirishwa

Turf Nmoor Wafanyakazi wa Uwanja wa Turf Moor wakijaribu lkuondoa barafu iliyodondoka kwa wingi uwanjani

Mon, 29 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mechi ya Burnley dhidi ya Tottenham iliyokuwa ichezwe katika dimba la Turf Moor jumapili jioni iliahiirishwa kutokana na kuanguka kwa kiasi kikubwa cha barafu uwanjani.

Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kwamba ni lini mchezo huo utachezwa, tangazo la kuharishwa kwa mechi hiyo lilifanyika mara baada ya pande zote mbili kutaja vikosi vyao kuelekea mchezo huo.

Spurs walikuwa wamechelewa kufika uwanja wa Turf Moor, walifika zaidi ya saa moja kabla ya mechi kuanza, na maafisa walikuwa wamesubiri hadi mameneja wote wawili wawepo kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho.

Joto la chini la ardhi la Turf Moor lilikuwa limewashwa kwa usiku mmoja lakini halikuweza kukabiliana na hali hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live