Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uvimbe kwenye ubongo wamtesa Dikembe Mutombo

Dikembe Mutombo Uvimbe kwenye ubongo wamtesa Dikembe Mutombo

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa NBA mwenye asili ya Congo, Dikembe Mutombo (56) anapatiwa matibabu katika jimbo la Atlanta kutokana na uvimbe wa kwenye ubongo.

Kwa mujibu wa ujumbe kutoka kwa familia yake ambao uliwasilishwa na afisa wa NBA Adam Silver, nyota huyo wa zamani wa mpira wa kikapu anapatiwa matibabu mazuri na ya juu na timu ya wataalamu,waliobobea.

Dikembe na familia yake wameomba kupewa faragha wakati huu ili waweze kuzingatia zaidi matibabu yake, pia wanawashukuru watu wote kwa maombi yao na salamu za kumtakia afya njema.

Nyota huyo alizaliwa Congo na kuhamia Marekani mwaka 1987 kwa ajili ya masomo katika Chuo Kikuu cha Georgetown, alipata umaarufu mwaka mmoja baadae baada ya kujiunga na timu ya mpira wa kikapu.

Amewahi kuchezea timu tofauti katika majimbo mbalimbali nchini Marekani na alistaafu mwaka 1999.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live