Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Utu lazima ushinde' katika mzozo wa Israel na Gaza - Salah

C7a5eef2 3491 437f B81e 71fb5d4f01e9.png 'Utu lazima ushinde' katika mzozo wa Israel na Gaza - Salah

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Mshambulizi wa Liverpool na Misri Mohamed Salah ametoa wito kwa "viongozi wa dunia kukutana pamoja ili kuzuia mauaji zaidi ya nafsi zisizo na hatia" huku mzozo wa Israel na Gaza ukiendelea.

Salah, 31, alisema msaada wa kibinadamu kwa Gaza lazima uruhusiwe "mara moja".

"Kumekuwa na vurugu nyingi, huzuni na ukatili," alisema kwenye video iliyowekwa kwenye mtandao wa X.

"Watu wa Gaza wanahitaji chakula, maji na vifaa vya matibabu kwa dharura.

"Maisha yote ni muhimu na lazima yalindwe. Mauaji yanapaswa kukomeshwa. Familia zinasambaratika.

"Ninatoa wito kwa viongozi wa ulimwengu kukusanyika ili kuzuia mauaji zaidi ya nafsi zisizo na hatia.

"Ubinadamu lazima ushinde."

Chanzo: Bbc