Baada ya Mshambuliaji wa Simba SC, Jean Othos Baleke kuonekana kwenye ndege na kudhaniwa kuwa mbioni kuondoka klabuni hapo ripoti zinadai kuwa amerejea nyumbani kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa ajili ya kubadilisha pasi yake ya kusafiria (PASPORT).
Moja ya Kiongozi wa Simba SC ameripotiwa kuwatoa wasiwasi mashabiki kwamba Mkongomani huyo hawezi kuondoka Simba SC na kubainisha kuwa passport yake imejaa hivyo imemnyima nafasi ya kuingia Uturuki ambako klabu hiyo inakwenda kufanya maandalizi ya msimu mpya.
“Baleke hawezi kuondoka Simba SC ila tu anarejea nyumbani kwao kwenda kubadilisha PASPORT yake ambayo imejaa kwa hivyo amekosa Visa ya kuingia nchini Uturuki ila akishabadilisha Pasi yake ya Kusafiria na kupata Visa ataungana na wenzake ambao wataoondoka nchini Jumanne ya Julai 11." - ameripitiwa alisema kiongozi huyo.
Baleke (22) aliposti picha kwenye Insta-Story yake akiwa kwenye ndege huku kukiwa na maandishi ya kutatanisha yaliyosomeka “GOOD BAY TANZANIA” na kudhaniwa kuwa huenda alikosea kuandika ‘Bay’ badala ya ‘bye’ kwa maana ya “Good bye Tanzania” yenye maana ya kwaheri Tanzania.