Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utata mtupu kifo cha kocha Simba

Zrane Maja (4).jpeg Kocha Zrane enzi za uhai wake na makocha wenzake

Tue, 2 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa viungo wa zamani wa Klabu ya Simba, Adel Zrane amefariki dunia huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakijafahamika.

Kwa mujibu wa klabu aliyokuwa akiifundisha kabla ya mauti kumfika, APR ya nchini Rwanda, imethibitisha kifo cha kocha huyo kupitia mtandao wa kijamii Instagram!.

"Tunasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa kocha wetu wa viungo Zrane, sababu ya kifo chake bado haijafahamika. Pumzika kwa amani," inasomeka hivyo taarifa ya APR.

MASTAA WAMLILIA Wakimzungumzia kocha huyo wachezaji mbalimbali wamezungumzia nafasi waliyopata kushirikiana naye enzi za uhai wake, huku wengine wakionyesha tu kuumizwa na kifo chake.

Kiungo mkabaji wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa anakipiga APR, Taddeo Lwanga ameposti picha kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram na kuandika 'Maisha ni mafupi, tumezungumza jana, sikufahamu kama utakutana na aliyekuumba leo. Pumzika kwa amani rafiki."

Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Singida Fountain Gate na sasa Namungo, Meddie Kagere ameandika 'Ni habari mbaya pumzika kwa amani kaka yangu Zrane kila siku nitakukumbuka."

Zrane ambaye alipita Simba akosaidiana na kocha mkuu Mfaransa Didier Gomes Da Rosa pamoja na aliyekuwa kocha wa makipa Mbrazili Milton Nienov kwa pamoja waliachana na timu hiyo baada ya kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika msimu wa 2021-22.

Kabla ya kifo chake Zrane alipoondoka Simba aliandika: "Kwa masikitiko makubwa naondoka nchi niipendayo Tanzania. Yametimia. Muda umekwisha. Naipenda Tanzania nawatakia kila la heri watu wote na utawala wake.

"Tanzania itakuwa kimbilio langu la kwanza kwa likizo. Nawapenda wote na asante kwa misimu yote minne iliyopita. Mmekuwa familia yangu ya pili, nawapenda na kuwaheshimu wote."

Akiwa na Simba amefanya kazi na makocha tofauti akianza na Patrick Aussems, Sven Vandebroeck na Didier Gomes ambapo alikuwa kipenzi cha mashabiki kwa namna alivyoifanya timu hiyo kuwa kwenye fiziki nzuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live