Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utata kuondolewa kwa viongozi Mbeya City

Mbeya City Kushuka Wachezaji wa Mbeya City

Thu, 18 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya uongozi kukanusha vikali, lakini Mwanaspoti imethibitishiwa Mbeya City kuwatimua kazi viongozi watatu wa benchi la ufundi huku sababu zikiwa hazijawekwa wazi.

Mbeya City inayohaha kusaka matokeo mazuri kwa sasa, inajindaa na mechi mbili za mwisho dhidi ya Yanga na KMC kumaliza msimu na kusubiri hatma yao ya kubaki au kushuka daraja.

Habari ilizopata gazeti hili ni kuwa kocha msaidizi, Anthony Mwamlima, kocha wa makipa, Ally Mustafa ‘Bartez’ na daktari wao Omary Stanley wote wametimuliwa kazi huku sababu zikiwa hazijulikani.

Aliyekuwa daktari wa timu hiyo, Stanley alithibitisha kutokuwa kikosini tangu City ilipokuwa ikijiandaa na mchezo wake dhidi ya Geita Gold akifafanua walifikia makubaliano na mabosi wa timu hiyo.

“Nadhani ni ishu ya mtu binafsi kuamua kushawishi uongozi kutuacha, mkataba wangu ulikuwa uishe mwishoni mwa msimu huu ila waliamua kuvunja hivyo kwa sasa nipo nyumbani nasubiri sehemu nyingine itakayonihitaji,” alisema Stanley aliyewahi kuhudumu Mbeya Kwanza.

Naye kocha msaidizi, Mwamlima alikiri kutokuwa kikosini humo akieleza hata mchezo uliopita dhidi ya Geita Gold hakuwa sehemu ya benchi la ufundi na mechi ya mwisho kwake ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar.

“Mkataba wangu ulikuwa wa kila mwaka lakini hadi safari ya Geita sikuwepo kikosini licha ya maandalizi yote kushiriki hivyo niliitwa na uongozi tukapeana mkono wa kwa kheri” alisema kocha huyo wa zamani wa Ken Gold.

Mtendaji mkuu wa timu hiyo, Emanuel Kimbe alisema hakuna taarifa zozote za namna hiyo na badala yake kwa sasa wapo bize kujiandaa na mechi mbili zilizobaki kuhakikisha City inabaki salama ligi kuu.

“Hakuna kitu kama hicho, timu imefika usiku wa kuamkia leo Jumanne (jana) na tunaendelea na mipango mikakati ya kujiandaa tena na mechi hizi zilizobaki,” alisema Kimbe.

Chanzo: Mwanaspoti