Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utata, figisu Tuzo za TFF

Bocco Tuzo Mchezaji Bora Ligi Kuu , John Bocco

Fri, 22 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usiku wa Oktoba 21, zilitolewa Tuzo za TFF kwa wachezaji, Makocha na Timu zilizofanya vyema kwa msimu uliopita wa 2020/2021.

Tuzo hizo zilihusisha mashindano yote kuanzia Ligi Kuu mpaka kombe la Ligi, ikihusisha Ligi ya wanawake na Wanaume.

Lakini kuna baadhi ya vipengele ambavyo wapenzi, wadau na wafuatiliaji wa masuala ya Soka wameonekana kukosoa na kuona pengine labda kuna figisu katika utolewaji wake.

Tuzo ya Mchezaji Bora Ligi Kuu Bara

Hii imekwenda kwa nahodha wa Simba, John Bocco, lakini msimu uliopita ndani ya kikosi hicho kulikuwa na mtu anayeitwa Clatous Chotta Chama, ambae kwa sasa ametimkia nchini Morocco.

Wengi wanaamini kiungo huyo wa Zambia alistahili kubeba tuzo hiyo kwa mchango mkubwa aliouonesha kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu na Kombe la Ligi.

Chama amepika idadi kubwa ya magoli, amefunga, na yeye mwenyewe alikua kiunganishi wa timu. Timu ilicheza kumtegemea yeye.

Tuzo ya Kocha Bora Ligi ya Wanawake ya Serengeti Lite

Alieibuka mshindi ni Edna Lema, lakini Simba queens walitwaa ubingwa ligi ya wanawake bila kupoteza mchezo hata mmoja. Cha kushtua, Mussa Mgosi kocha wa Simba Queens, hajatwaa tuzo ya kocha bora wa msimu wanawake. Tulitaka afanye nini zaidi

Tuzo ya Mchezaji bora wa Kombe la Azam

Hapa kiungo wa Yanga Feisal Salum "Fei Toto" ameibuka kidedea lakini walio wengi wanampa heshima ya tuzo hiyo aliekua kiungo mshambuliaji wa Simba ambae kwa sasa ametimkia klabu ya Al Ahly ya Misri.

Wengi wameheshimu sana alichokifanya Fey Toto FA, lakini TFF wamelalamikiwa kufumba macho kwa kutaka kuweka mzani sawa. Luis Miquissone ameibiwa tuzo yake. Alikuwa na maajabu kuliko Fei Toto. Labda amenyongwa kwasababu hayupo nchini.

Tuzo ya muhamasishaji Bora

Hii ilikwenda kwa Nick Leonard, maarufu kwa jina la “Bongo Zozo”. Muhamasishaji bora, kama Antonio Nugaz hakuwa katika kinyang'anyiro, tuzo haikustahili kuwa na mpinzani tena. Mshindi ni Haji Manara. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Takwimu za Bodi ya Ligi wiki chache zilizopita ilionesha Mashabiki wa Yanga ndio walioongoza kwa kuhudhuria viwanjani lakini cha ajabu Nugaz hata jina lake halikuwemo.

Mpinzani wake wa karibu, Haji Manara ndio aliepaswa kubeba tuzo ile kwa namna alivyokuwa akiwahamasihsa mashabiki wa Simba kuhudhuria viwanjani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live