Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utamu wa Ligi Kuu England umefika mwisho, balaa ni kubwa

IMG 4151 Celebration.jpeg Mabingwa wa EPL, 2022/23

Sat, 27 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ile filamu tamu ya Ligi Kuu England imefika mwisho, ambapo kesho Jumapili zitapigwa mechi za kuhitimisha msimu wa 2022/23. Mechi 10 kwenye viwanja 10 tofauti zitapigwa muda mmoja, saa 12:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Ligi inamalizika huku bingwa akiwa ni Manchester City na tayari timu nne zitakazoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa msimu ujao zishapatikana sawa na ilivyo kwa timu zitakazoshiriki michuano ya Europa League pia.

Ukiondoa haya bado kuna baadhi ya vita hazijaamuliwa hadi sasa na zinatarajiwa kupatiwa ufumbuzi kwenye mechi za kesho kulingana na matokeo yatakavyokuwa. Hapa tumekuchambulia kwa kina baadhi ya vita zilizosalia ambazo zitaamuliwa kwenye mechi hizi za mwisho.

KUSHUKA DARAJA

Ukiiondoa Southampton ambayo tayari imeshashuka daraja, kuna Leeds United iliyo nafasi ya 19 ikiwa na pointi 31, Leicester City nafasi ya 18 ikiwa na pointi 31 na Everton iliyo nafasi ya 17 kwa pointi zao 33, zote hizi zinaweza kuungana na Southampton kwenye ligi daraja a kwanza msimu ujao.

Hili linawezekana ikiwa Everton itapoteza mchezo wao wa mwisho dhidi ya Bournemouth ambayo inashika nafasi ya 15 ikiwa na alama 39 na ikiwa itashinda mechi hii na Wolves, West Ham zikipoteza itakuwa imepaa hadi nafasi ya 13.

Hata hivyo uwezekano wa kubaki kwa Leeds United unaonekana kuwa mdogo kwa sababu mchezo wa mwisho itakutana na Tottenham ambayo itataka kushinda mechi hii na kuiombea mabaya Aston Villa ili wafuzu kucheza michuano ya Europa Conference League mwakani.

Kwa upande wa Leicester City ambayo itakutana na West Ham inaonekana kidogo kuwa na mfupa rahisi kwani wapinzani wao hao watahitaji kupumzisha wachezaji wengi kwa ajili ya fainali ya michuano ya Europa Conference League ambapo itacheza dhidi ya...

VITA YA EUROPA CONFERENCE LEAGUE

Hapa kuna timu tatu zinazopambana kwenye vita hii, kwanza kabisa ni Aston Villa ambayo inaonekana kuwa na asilimia nyingi kwani inaashika nafasi ya saba ikiwa na pointi 58, ikifuatiwa na Tottenham iliyo nafasi ya nane ikiwa na pointi 57, sambamba na Brenford iliyopo nafasi ya tisa kwa pointi zao 56.

Brentford na Spurs zinatakiwa zishinde mechi zao kisha ziombee Aston Villa ipoteze ili ziweze kumshusha kwenye nafasi yake ya sasa.

Brentford atakuwa na kibarua kigumu kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Manchester City wakati Spurs ikiumana na Leeds United huku Aston Villa ambayo inaombewa mabaya itakuwa nyumbani pia kuvaana na vijana wa fundi wa mifumo na mbinu Roberto De Zerbi.

VITA YA SH6.3BILIONI

Ukiondoa vita tajwa hapo juu, timu sita zinazoshika nafasi 11 hadu 16 zenyewe zitakuwa na vita yao tofauti ya kugombania Pauni 2.2 milioni ambayo ni sawa na bilioni 6.3 kwa pesa za kibongo.

Kiasi hiki cha pesa kinatokana na aina ya nafasi ambazo watamaliza. Kawaida utaratibu wa Ligi Kuu England upo hivi, wakati msimu unaanza pesa ya haki ya matangazo ya televisheni hugaiwa kwa mafungu matatu.

Fungu la kwanza hutolewa asilimia 50 ya pesa yote kwa ujumla na kila timu hupewa, kisha asilimia 25 hutolewa kulingana na mechi ambazo zimeonyeshwa kwenye televisheni na asilimia 25 hutolewa kulingana na nafasi timu zimemaliza.

Sasa kila unapozidi kumaliza nafasi ya juu kwenye mgawanyo wako huongezeka Pauni 2.2 milioni pesa ambazo ni nyingi hivyo timu hizi mbali yakuwa zimejihakikishia kutoshuka daraja zitataka kushinda na kuziombea timu zilizo juu yao mabaya.

Hapa kuna Crystal Palace yenye alama 44 ambayo itatakiwa kushinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Nottingham Forest ili isishushwe na Chelsea yenye pointi 43.

Chelsea ambayo itamaliza na Newcastle nyumhani itatakiwa kushinda mechi ili isishushwe na Wolves inayoifuatia kwenye nafasi ya 13 na pointi zao 41.

West Ham iliyo nafasi ya 14 kwa pointi 40 itatakiwa kuifunga Leicester City ili isishushwe na Bournemouth iliyo nafasi ya 15 na pointi zao 39.

Nottingham Forest ambayo imetoka kuikosesha ubingwa Arsenal itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Cryastal Palace ambayo pia inataka kushinda ili kuendelea kusalia nafasi iliyopo.

RATIBA YOTE JUMAPILI, MEI 28

Arsenal v Wolves (12:30 jioni) Aston Villa v Brighton (12:30 jioni) Brentford v Man City (12:30 jioni) Chelsea v Newcastle United (12:30 jioni) Crystal Palace v Notti'm Forest (12:30 jioni) Everton v Bournemouth (12:30 jioni) Leeds United v Tottenham (12:30 jioni) Leicester City v West Ham (12:30 jioni) Man United v Fulham (12:30 jioni) Southampton v Liverpool (12:30 jioni)

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: