Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utambulisho wa Ulimwengu Singida FG umestua hapa

Ert Thomas Ulimwengu Sa Thomas Ulimwengu

Thu, 3 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Singida Fountain Gate imemtambulisha mshambuliaji wa zamani wa TP Mazembe Thomas Ulimwengu kuwa mchezaji wao mpya katika Singida Big Day jana Agosti 2 kwenye uwanja wa Liti Mkoani Singida ambapo walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya AS Vita ya DR Congo.

Usajili wa Thomas umeshtua kwa sababu ya mambo kadhaa, moja ni kwamba hakuwahi kucheza kwenye klabu za Tanzania kwenye ligi yetu, kwahiyo wengi walikuwa wanatamani kuona siku ambayo atacheza ni atacheza timu gani, na wengi sana waliwaza huenda atahusishwa na Simba,Yanga na Azam lakini haikuwa hivyo, lakini mwishoni za kikachero zilienea kwamba ataibukia Singida Fountain Gate.

Kila shabiki anasubiri kuona Ulimwengu amerudi na kitu gani katika Ligi yetu kuelekea msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live