Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utambulisho wa Mourinho wafunika Fenerbahce

Fenerbahce Mourinho.jpeg Utambulisho wa Mourinho wafunika Fenerbahce

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maelfu ya mashabiki wa klabu ya Fenerbahce jana walijitokeza katika mapokezi ya kocha wao mpya, Jose Mourinho wakati akitambuliwa kwenye Uwanja wa Sukru Saracoglu Jijini la Istanbul, Jana Juni 2, 2024

Kocha huyo amerejea katika majukumu hayo ikiwa ni miezi mitano tangu alipofukuzwa katika Klabu ya Roma ya Italia. Baada ya kutambulishwa akiwa na jezi ya Fenerbahce, Mourinho amesema “Hii jezi sasa ni ngozi yangu, ndoto zenu ni ndoto zangu”

Mourinho (61) ambaye alianza Majukumu ya kuwa Kocha Mkuu Mwaka 2000, ameshazitumikia Benfica, Uniao de Leiria, Porto, Chelsea, Inter Milan, Real Madrid, Manchester United, Tottenham Hotspur na Roma

Chanzo: www.tanzaniaweb.live