Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utambulisho wa Mbappe Real Madrid kufuru

Mbappe Kufuru Utambulisho wa Mbappe Real Madrid kufuru

Mon, 15 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Tiketi za kwenda kumshuhudia Kylian Mbappe katika siku ya utambulisho wake kesho kwenye dimba la Santiago Bernabeu zimeripotiwa kuisha ndani ya muda mfupi tu baada ya kuanza kuuzwa huku baadhi ya vishoka wakiziuza tena kwa zaidi ya Euro 200.

Real Madrid ilikuwa ikizigawa tiketi bure kabisa kwa wanachama wake kupitia tovuti yao na baadhi yao wakatumia fursa hiyo kuchukua tiketi hizo na kuanza kuziuza.

Bei ya tiketi hizo inaripotiwa kuanzia Euro 30 hadi 200, ikitegemea na jukwaa.

Zaidi ya mashabikii 100,000 wameripotiwa kuingia katika tovuti ya Madrid kwa ajili ya kujichukulia tiketi ikiwa ni namba iliyozidi hadi uwezo wa uwanja wa Bernabeu ambao unaingiza mashabiki 85,000 tu.

Mashabiki wengi wameonyesha kuchukizwa na hali ya kukosa tiketi na kueleza hisia zao katika mitandao ya kijamii wakisema kuna udanganyifu umefanyika.

"Tiketi kwa ajili ya kutazama utambulisho wa Kylian Mbappe ziliwekwa katika tovuti na ndani ya muda mchache mashabiki ambao hata hawatokwenda uwanjani walizichukua na kuanza kuziuza upya kwa bei kubwa,"alisema shabiki mmoja kupitia Twitter.

Shabiki mwingine naye akasem:" Ni aibu kuwa na mashabiki wenye tabia kama hii, timu itabidi aingalie namna ya kuwafutia tiketi wale wote wanaoziuza."

Utambulisho wa Mbappe huenda ukavunja rekodi kwa kuhudhuriwa na watu wengi zaidi, mchezaji wa mwisho kuhudhuriwa na mashabiki wengi wa timu hiyo siku ya utambulisho wake ilikuwa ni Cristiano Ronaldo ambao walikuwa ni 80,000.

Suala la tiketi za kwenda kumshuhudia limeibuka ikiwa ni siku chache tu baada ya kuripotiwa kwamba jezi zake zimenunuliwa kwa haraka na sasa ukiagiza itakuhitaji usubiri walau kwa wiki nne hadi sita ili kuipata.

Chanzo: Mwanaspoti