Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utambulisho wa Chama kuvunja rekodi

Chama Msz Utambulisho wa Chama kuvunja rekodi

Wed, 3 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imepanga kumtambulisha kiungo wao mpya Clatous Chama kwa ukubwa unaoendana na usajili wenyewe.

Kitengo cha Yanga cha Ubunifu na Masoko kinapaswa kuchemsha ubongo vizuri ili kuinufaisha klabu hiyo kibiashara.

"Suala la Usajili wa Chama ni sehemu ya biashara yetu. Kila mtu anakiri kuwa usajili wa Chama ni usajili mkubwa. Najua wengi wanauliza kwanini hatujamtambulisha Chama na jezi ya Yanga."

"Mtiririko wa matukio ya usajili huu wa Chama kwetu ni fursa. Najua wengi wanatamani kujua," amesema Ally Kamwe, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Yanga.

Kutokana na trend ilivyo kwa sasa ambapo mashabiki wanashauku ya kumuona Chama akiwa ndani ya uzi wa Yanga.

Zikichapishwa jezi mpya mapema kisha wakatangaza kuwa, kuna jezi maalumu za Clatous Chama, kila jezi Tsh 50,000, watapiga sana pesa.

Huenda pesa iliyotumika kumsajili kiungo huyo ikarudi na kuzidi ndani ya siku moja tu baada ya utambulisho wake.

Mfano: Wakichapisha jezi elfu 20 pekee wakaziuza kwa Tsh 50,000 kila jezi Nchi Nzima, klabu ya Yanga itaingiza kiasi cha Tsh bilioni 1.

Peleka jezi elfu tatu (3,000) tu katika kila mkoa kwenye mikoa (7) yenye nguvu kiuchumi Tanzania, jezi zinaisha siku moja tu. 3000 × 7 = 21,000 jezi.

Chama anaweza kuinufaisha Yanga ndani ya uwanja na hata nje ya uwanja. Pia, kuna Prince Dube, utambulisho wake haupaswi kufanyika bila kuinufaisha Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: