Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utake usitake Azam Bingwa 2024/25

Kipre Azam Fc Wachezaji wa Azam FC

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimu wa ligi kuu ya NBC 2023/24 utakamilika leo jioni kwa timu zote 16 kushuka kwenye madimba nane tofauti katika muda mmoja wa saa kumi alasiri.

Tayari bingwa alishapatikana lakini ligi bado ina msisimko mkubwa sana kwa mbio za kuwania nafasi ya pili, kuwepa kushuka daraja na kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora.

Hayo yote yatakajulikana leo jioni baada ya filimbi za mwisho katika michezo yote.

Kukamilika kwa msimu huu ndiyo kuanza maandalizi kwa msimu ujao, na tukizungumzia maandalizi, Azam FC ndiyo timu iliyoanza mapema zaidi.

Imekuwa ikitambulisha wachezaji wapya tangu mwezi Machi, wakianza na Yoro Diaby, mlinzi raia wa Mali kutoka klabu ya Stade Malien alikokuwa kwa mkopo kutoka akademi ya Yeleen Olympique ya Mali.

Baadaye akatambulishwa Frank Tiesse kutoka timu hiyo hiyo, raia wa Ivory Coast aliyerithi kitambaa cha unahodha klabuni hapo kutoka kwa Djigui Diarra.

Tukielekea kukamilisha msimu, wametambulisha wengine wawili kutoka Colombia; kiungo Ever Meza na mshambuliaji wa kati, Jhonier Blanco.

Na inasemekana hawajamaliza, bado kuna vyuma vinakuja.Haya yote ni maandalizi ya msimu ujao ikiashiria kwamba Azam FC kuna jambo wanalitafuta msimu ujao.

Ukiangalia matokeo yao kwa misimu mitatu iliyopita, kuanzia 2021/22 pale ligi yetu ilipoanza kuwa na timu 16 kutoka 18 za msimu wa nyuma yake, utaona Azam FC inaimarika kidogo kidogo.

2023/24 MP W D L GF GA GD PTS 29 20 6 3 61 21 +40 66

2022/23 MP W D L GF GA GD PTS 30 18 5 7 55 29 +26 59

2021/22 MP W D L GF GA GD PTS 30 14 7 9 41 28 +13 49

Wakishinda mchezo wa mwisho dhidi ya Geita, Gold, watafikisha alama 69. Hili ni ongezeko la alama 10 kutoka msimu uliopita.

Ukiangalia ‘hii trend’ utaona wamekuwa wakiongeza alama 10 kila msimu.

2021/22 -Alama 49

2022/23 -Alama 59

2023/24 -Alama 69*

Endapo msimu ujao wataongeza tena alama 10 maana yake watakuwa na alama 79. Hizo ndizo alama za mabingwa kila msimu tangu ligi iwe na timu 16.

2021/22 -Yanga alama 74

2022/23 -Yanga alama 78

2023/24 -Yanga alama 77*

NB Yanga walitangaza ubingwa kwa alama 71 tu.Ukiangalia rekodi za Azam FC katika misimu mitatu kwa kulinganiha na huu, utaona mabadiliko makubwa sana.

Msimu huu wamefunga mabao mengi zaidi hadi sasa - 61. Msimu huu wamefungwa mabao machache zaidi hadi sasa - 21. Msimu huu wamevuna alama nyingi zaidi hadi sasa - 66. Msimu huu wameshinda mechi nyingi zaidi hadi sasa - 20. Msimu huu wamepoteza mechi chache zaidi hadi sasa - 3. Wasomi wanasema namba hazidanganyi, na kwa namba hizi za Azam FC, ni dhahiri kwamba kuna kitu ambacho wanaweza kufanya msimu ujao.

Ukichukua haya yote ukachanganya na aina ya wachezaji wanaosajiliwa, utanielewa.

1. Yoro Mamadou Diaby

Ni zao la akademi ya Yeleen Olympique ya Mali, ambayo ni maarufu sana kwa kuzalisha vipaji.

Alizaliwa Februri 11, 2001 na sasa ana miaka 23. Amezichezea timu zote za taifa za vijana za Mali, kuanzia ile ya chini ya miaka 17, chini ya miaka 20 na chini ya miaka 23.

Pia aliichezea timu ya taifa ya CHAN, akiwa nahodha msaidizi katika mashindano yaliyofanyika Algeria.

Katika mashindano hayo, Yoro alikuwa mchezaji bora kwenye mechi dhidi ya Angola, iliyoisha kwa sare ya 3-3.

Wakiwa nyuma 3-0 Mali walirudi kwa kishindo na kusawazisha, Yoro alifunga bao la kwanza dakika ya 72.

Akiwa na klabu yake ya Stade Malien, aliisaidia kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho, akifunga mabao katika mechi zote mbili za robo fainali, japo timu yake ilitolewa.

Mechi ya kwanza nyumbani iliisha kwa sare ya 1-1 na ugenini wakafungwa 2-1. Mabao yote ya timu yake akifunga yeye.

2. Frank Tiesse

Ni raia wa Ivory Coast ambaye alicheza na Kipre Jr. kwenye klabu moja ya Sol FC (Stars Olympic FC) ya Ivory Coast.

Alizaliwa Disemba 17, 1997, akiwa na miaka 26 sasa. Yeye ndiyo nahodha wa Stade Malien na alikuwa mmoja wa wachezaji bora wa mashindano ya Kombe la Shirikisho.

Kwa mujibu wa ntandao ya FootMob, Tiesse alitengeneza nafasi 15 za mabao katika mechi 7 za Kombe la Shirikisho alizocheza. Hizi ni nafasi nyingi zaidi katika mashindano ya msimu hui. Pia alifanikiwa kukokota mipira (dribles) mara nyingi zaidi na kuongoza kwenye mashindano ya msimu huu. Kwa kifupi Tiesse ni zaidi ya Kipre Junior kwenye kutembea na mipira.

Kama unadhani Kipre Jr. ni noma kwenye kupenya penya, basi huyu ni mara 10 zaidi yake.

3. Ever Meza

Kiungo wa mpira mwenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 8. Jina lake kamili ni Ever William Meza Mercado. Alizaliwa Julai 21, 2000 huko Colombia.

Anacheza nafasi zote za kiungo na hata beki wa kati na pembeni. Ana uzoefu wa kucheza mashindano makubwa ya Copa Sudamericana, ambayo ni sawa na Kombe la Shirikisho la CAF kwa hapa Afrika.

Alikuwa mchezaji wa timu ya Leonnes FC ambayo ilishuka daraja kwenye ligi kuu ya Colombia.

Timu ikashuka lakini yeye hakushuka, akachukuliwa kwa mkopo kwenye timu ya Alianza FC ambayo ndiyo aliitumikia msimu huu unaoisha.

Akiwa na timu hii ndiyo akashiriki Copa Sudamericana. Kama ambavyo jina lake linavyosomeka, MEZA, na maana yake ni hiyo hiyo kama ilivyo kwa Kiswahili.

4. Jhonier Blanco

Mfungaji bora wa ligi darsja la kwanza Colombia. Jamaa anajua kufunga, anajua kutafuta bao.

Jina lake kamili ni Jhonier Alfonso Blanco Yus. Alizaliwa Oktoba 18, 2000 huko Colombia na anakuja Tanzania akitokea klabu ya Aguilas.

Msimu uliopita, akiwa klabu ya Fortaleza, Blanco alikuwa mfungaji bora wa ligi daraja la kwanza ya Colombia, akiwa na mabao 13. Mtiririko unaonesha, usajili unaonesha…tusubiri uwanjani kuona kama yaliyomo yamo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live