Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usyk na Joshua kurudiana Agosti 2022

OLEKSANDR Joshua akimsukumia konde Usyk kwenye pambano lililopita mwaka 2021

Fri, 10 Jun 2022 Chanzo: eatv.tv

Pambano la masumbwi la marudiano la kuwania mikanda ya Ubingwa wa WBO, IBF na WBA kati ya bondia wa Ukraine Oleksandr Usyk na Anthony Joshua wa England linataraji kufanyika mwezi Agosti 2022 nchini Saudi Arabia baada ya kimya cha muda mrefu.

Ikumbukwe wawili hao walizichapa mwezi Septemba 2021 kwenye ulingo uliowekwa kwenye uwanja wa Tottenham Hotspurs na bondi Usyk kuibuka na ushindi na kubeba mikanda ya Ubingwa ya WBO, IBF na WBA.

Moja ya sababu iliyopelekea pambano hilo kuchelewa kufanyika mwezi Mei 2022 kama walitaraji, ni hali ya mapigano yaliyo nchini Ukraine anapotoka bondia Usyk ambaye na yeye alilazimika kujiunga na majeshi ya nchini humo kujihami dhidi ya Urusi.

Pambano hilo linasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa ndondi Ulimwenguni limeanza kutiliwa mashaka kufanyika nchini Saudi Arabia kutokana na nchi hiyo kutuhumiwa kuwa na desturi ya kukiuka haki za kibinadamu licha ya kuandaa pambano la Anthony Joshua alishinda mbele ya Andy Ruiz JR mwaka 2019.

Chanzo: eatv.tv