Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usiwapimie EPL wana mapafu ya mbwa

Dejan Kulusevski Dejan Kulusevski

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Msimu wa Ligi Kuu England ulianza kwa kasi kasi huku tukishuhudia timu zikichuana vikali nyingine zikipokea vichapo. Manchester City, Arsenal, Liverpool, Tottenham, Brighton, zimeendelea kutoa dozi kwa timu pinzani zikiwa hazijapoteza mechi tofauti na Chelsea na Manchester United ambazo tayari zimechezea kichapo.

Kwa mujibu wa utafiti, wachezaji kadhaa walionyesha viwango bora na wamekuwa na mchango mkubwa kwa klabu zao kutokana na uchapakazi wao wanapokuwa uwanjani. Kulingana na takwimu, baada ya mechi nne za ligi nyota wa

Tottenham, Dejan Kulusevski ndiye mchezaji aliyeonyesha bidii zaidi hadi sasa akihaha uwanja mzima - yaani kitaani tunasema ana mapafu ya mbwa.

Winga huyo wa Tottenham ameibuka kileleni mwa orodha ya wachapakazi akiwa na mikimbio mingi zaidi uwanjani ambayo ikiijumlisha kwa pamoja ni sawa na amekimbia kilometa 47.07. Katika mechi nne za mwanzo kwenye ligi nyota huyo wa kimataifa wa Sweden alihaha uwanjani akiisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester United.

Umbali huo unajumuisha kilometa 13 za mchango wake alitoa katika ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Bournemouth, mechi ambayo Kulusevski alifunga. Winga huyo pia aliibuka kuwa kinara katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sheffield United baada ya kuwa nyuma kwa bao 1-0.

Licha ya kuanza msimu vibaya akiwa na klabu yake ya Manchester United, Bruno Fernandes amekuwa na mchango mkubwa binafsi akishika nafasi ya pili kwenye urodha hiyo akiwa amezunguka uwanjani kwa kilometa 46.84 akifuatiwa na Declan Rice anayekamilisha tatu bora akiwa amekimbia kilomita 46.75. Bruno alikuwa na wikiendi mbovu kwani walipokea kichapo kingine cha mabao 3-1 dhidi ya Brighton katika mechi yao ya tano ya ligi baada ya kichapo kama hicho walichopata dhidi ya Arsenal kabla ya ligi kusimama.

Viungo hao (Bruno na Rice) walicheza dakika zote katika mechi nne za kwanza za ligi. Bruno, ambaye ni nahodha wa Man United alifunga bao na kutoa asisti katika mechi hizo.

Kwa upande wa Rice, alifunga bao lake la kwanza tangu ajiunge na Arsenal kutoka West Ham katika ushindi wao wa 3-1 dhidi ya Man United mapema mwezi huu.

Katika orodha hiyo, kiungo wa Man City, Rodri yuko nafasi ya tano akiwa amezunguka uwanjani kwa mikimbio ambayo ukiiunganisha pamoja inazaa umbali wa kilomita 46.37.

Mshindi wa Kombe la Dunia akiwa na timu ya taifa ya Argentina, Enzo Fernandez anayekipiga Chelsea anashika nafasi ya tisa akiwa na mikimbio inayozaa umbali wa jumla ya kilomita 45.19.

Orodha ya nyota wenye mapafu ya mbwa (na kwenye mabano kilometa walizokimbia baada ya mechi za mwanzo za EPL 2023-24):

1. Dejan Kulusevski- Tottenham (Umbali Kilometa 47.07)

2. Bruno Fernandes- Man United (Umbali kilometa 46.84)

3. Declan Rice- Arsenal- (Umbali kilometa 46.75)

4. Abdoulaye Doucouré - Everton (Umbali kilometa 46.43)

5. Rodri- Man City (Umbali kilometa 46.37)

6. Philip- Bournemouth (Umbali kilometa 45.97)

7. Bruno Guimares- Newcastle (Umbali kilometa 45.82)

8. Dominik Szoboszlai- Liverpool (Umbali kilometa 45.74)

9. Enzo Fernandes- Chelsea (Umbali kilometa 45.19)

10. Paschal Gross- Brighton (Umbali kilometa 44.77)

Chanzo: Mwanaspoti