Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Shaban Kamwe amesema kuwa kiu ya mshambuliaji wa timu hiyo, Fiston Mayele ni kuchukua kiatu cha mfungaji bora wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho CAF imebebwa na wachezaji wote na wapo tayari kumpa sapoti hiyo.
Kamwe amesema kuwa, kutokana na hilo, katika mchezo wa marudiano wa robo fainali dhidi ya Rivers United utakaopigwa Jumapili Aprili 23, 2023, hata golikipa Diarra anaweza kumpa assist Mayele ili afunge.
“Mayele wakati wako dressing room aliwaambia kwa mara ya kwanza naomba na nyie mkanisaidie nichukue hichi kiatu, inawezekana nikamaliza msimu nikiwa Top Scorer nyumbani na Top Scorer wa CAF Confederation.
“Ndio maana mnaona maassist wanaanzia nyuma, maishangae Dar es Salaam Diarra nae akapanda akamuekea Mayele assist,” Ally Kamwe.
Katika mchezo wa kwanza Yanga wakiwa ugenini, waliibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Rivers, assist zzote mbili zikitolewa na beki wa kati na nahodha wa timu hiyo, Bakari Nondo Mwamnyeto na kufungwa na Mayele.
Mayele amefikisha mabao 5 kwenye ligi hiyo ya CAFCC akiwa kinara wa upachikaji mabao mpaka sasa huku pia akiwa kinara wa mabao Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 16 na michezo minne ikiwa imesalia mkononi.