Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usiombe timu yako ikapangwa na Mamelodi Sundowns

Bafana Mamelodi Usiombe timu yako ikapangwa na Mamelodi Sundowns

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama ulikuwa unasikia jirani yako ataki timu yake ikutane na Mamelodi Sundowns na wewe ukamuona 'hamnazo' basi hamnazo wewe.

Bongo hhenda hakuna anaeiogopa (kuhiandafia) Mamelodi Sundowns lakini ukiwauliza Orlando Pirates au Kaizer Chiefs watakuambia mziki wa Mamelodi Sundowns.

Najua sisi Watanzania hatuna uoga wa kuiogopa Timu (inasaidia kufanya vizuri) lakini ukimuita Gadiel Michael au Baraka majogoro pamoja na Abdi Banda watakueleza ukali wa Mamelodi Sundowns.

Tuje katika kiini cha makala haya. Mamelodi wapo mbioni kushinda Kombe lao la (7) katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini kwa mfululizo, wewe huogopi tu?

Kuanzia Msimu wa (2017-18)(2018-19), (2019-20), (2020-21), (2021-2022), (2022-23) na sasa wanalisubiria la msimu huu wa 2023/24.

Msimamo wa Ligi Kuu Afrika Kusini Mamelodi Sundowns yuko kileleni akiwa na alama 45 akiwa na viporo Viwili (2). Ninapoandika makala haya, akifuatiwa na Orlando Pirates mwenye alama 33 nyuma yake Stellenbosch mwenye alama 32.

Usiseme Ligi ya Afrika Kusini haina ushindani sema Mamelodi Sundowns kawa wa hee! Msifie na anaekukimbiza basi.

Rekodi za Mamelodi kwenye michuano ya CAFCL tangu msimu wa mwaka 2016/2017;

2015 - Raundi ya kwanza

2016 - Bingwa

2017 - Robo Fainali

2018 - Hatua ya makundi

2018–19 - Nusu Fainali

2019–20 - Robo Fainali

2020–21 - Robo Fainali

2021–22 - Robo Fainali

2022–23 - Nusu Fainali.

Mamelodi ndiyo mabingwa wa michuano mipya ya African Football League (AFL) ambapo walimfunga Wydad Casablanca.

Juzi Mamelodi Sundowns kafikisha unbeaten 41 baada ya kumfunga Chippa United goli 2 kwa (0) Magoli ya Mamelodi yakifungwa na Mokena na Tashreeq Mathews.

Tukiwa tumebakisha saa chache kuelekea droo ya robo fainali Kombe la Klabu Bingwa (CAF) Omba sana timu yako isipangiwe na Mamelodi Sundowns, japo mpira unadunda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live