Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usiombe kukutana na Wagosi kwa sasa

Coastal Union Pic Usiombe kukutana na Wagosi kwa sasa

Sat, 8 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Coastal Union au Wagosi wa Kaya au Wanamangushi kwa sasa ina jambo lake ambalo ni kuhakikisha inabaki Ligi Kuu kwa hawapo pazuri kwenye msimamo.

Inapofika muda wa Coastal kupambania jambo lake, huwa inaonyesha wazi kuwa imedhamiria na mwishoni mara nyingi hufanikiwa.

Kwanza huko Tanga unaambiwa vigogo na wadau wa Coastal, vikao haviishi kila wakati wakijadiliana ni kwa namna gani timu yao inakwepa mtego wa kuangukia Ligi ya Championship.

Vikao kama hivyo ndivyo huibua masuala ya hamasa kwa wachezaji kama vile bonasi na posho ili kuwashawishi wapambane zaidi katika mechi walizobakiza nyumbani wapate matokeo mazuri ambayo yatawafanya wabaki Ligi Kuu.

Na usishangae kuona kipindi kama hiki wachezaji kulipwa madai yao yote na watakuwa wanalelewa vyema na uongozi kwa kupatiwa kwa haraka mahitaji yao ili mradi tu wawe sawa kisaikolojia na wacheze mechi wakiwa na utulivu kichwani.

Kuna maisha fulani ya tofauti huonekana ndani ya Coastal katika nyakati kama hizi ambao huwa wanapambana kuhakikisha hawashuki daraja.

Wote huwa na umoja kuanzia wachezaji, makocha, viongozi na mashabiki wao na tofauti zao za nyuma huziweka kando kuhakikisha timu inakuwa salama.

Wachezaji huonekana wana morali kubwa hasa wanapokuwa kwao Uwanja wa Mkwakwani kuhakikisha timu haipotezi wakitumia vyema makosa ya timu pinzani na hata ya waamuzi kuhakikisha timu yao inafanya vizuri.

Lakini kiuhalisia hayo yote yalipaswa kufanyika katika kipindi chote cha msimu pasipo kusubiria mechi hizi za mwisho wakiwa katika hatari ya kushuka daraja.

Wangekuwa wanakusanya pointi za mapema ambazo zingewapunguzia presha katika mechi hizi za mwishoni ambazo huwalazimisha watumie nguvu kubwa ili wabaki Ligi Kuu.

Inashangaza kila wanapokuwa katika hatari ya kushuka daraja ndio wanaona umuhimu wa kupambana kusaka pointi tatu katika kila mchezo lakini kinyume chake huwezi kuona hali kama hiyo.

Wakati kama huu Coastal huwa kama Al Ahly au Mamelodi Sundowns vile lakini katika nyakati za kawaida, huwa hawatofautiani na timu yangu ya mtaani ya Basihaya Arena ya kule Boko.

Chanzo: Mwanaspoti