Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usife kama mimi - George Best

George Best Mr Usife kama mimi - George Best

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

George Best, kwa waliobahatika kumshuhudia vizuri kwa miaka hiyo, wanasema ndie mchezaji bora katika historia ya Northern Ireland na pia ni moja kati ya malijendi wa klabu ya Manchester United.

Alizaliwa tarehe 22 Mei mwaka 1946 huko, Ireland ya Kaskazini .Anatajwa kama mmoja ya wachezaji bora kuwahi kutokea katika ulimwengu huu. Ni moja kati ya mawinga bora kuwahi kutokea, kwanzia kwenye kontroo, kupokea mipira kwa ustadi mkubwa, uwezo wa kupunguza mabeki na spidi.

Manchester United ndio sehemu alipotumia muda mwingi kutengeneza rekodi zake za kisoka, kwa sababu ndipo sehemu alipocheza kwa muda mrefu.

Best akiwa na umri wa miaka 22 tu, alikuwa tayari ameshinda tunzo ya Ballon d'Or ambapo aliipata 1968 na ndie aliekuwa nyota anaetazamwa zaidi kwa kipindi hicho

Akiwa na umri wa miaka 28 alishaifungia united jumla ya magoli 181 na kushinda mataji 6.

Pamoja na mafanikio hayo George Best alishindwa kuimili presha na umaarufu aliokuwa nao ndani ya uwanja na nje pia

Unywaji wa pombe kupitiliza na wanawake ndio ilikuwa starehe kubwa ya George best

Moja kati ya nukuu za George Best kuhusu ulevi na wanawake alisema "Mwaka 1969 niliacha kabisa matumizi ya pombe na wanawake, katika kipindi kifupi zilikuwa ni dakika 20 mbaya zaidi katika maisha yangu, nilianza kutumia tena fedha nyingi kwenye magari, pombe na wanawake, nilipoteza kila kitu"

Mwaka 2005, George Best kutokana na ulevi kupindukia ini lake lilipata shida na ndipo akakimbizwa hospitali,

Akijua nini kinafata kwake George alimuomba binti yake anunue sehemu ya tangazo katika gazeti moja na achapishe picha ya hali yake ya kiafya ikiwa na nukuu inayosema "Usife kama mimi"

Na siku 5 badae november 25 mwaka 2005 George Best alifariki akiwa na umri wa miaka 59.

Kijana unajifunza nini kwa historia hii ya George Best?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live