Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usichokijua kuhusu Kombe la Dunia timu za Klabu

Liverpool Captain Jordan Henderson Lifts The Fifa Club World Cup Usichokijua kuhusu Kombe la Dunia timu za Klabu

Tue, 19 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Shirikisho la kimataifa la vyama vya soka (FIFA) linatarajia kuandaa michuano mipya ya fainali za Kombe la Dunia kwa timu za klabu itakayoanza kufanyika 2025 huko Marekani.

Manchester City na Chelsea zitaiwakilisha Ligi Kuu England kwenye fainali hizo, ambapo Liverpool na Manchester United hata zifanyaje hazitaweza kufuzu kwa mikikimikiki hiyo ya 2025.

Real Madrid na Bayern Munich zimefuzu michuano hiyo baada ya kunyakua mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakati Paris Saint-Germain, Inter Milan, FC Porto na Benfica zenyewe zimepata nafasi kutokana na pointi zilizovuna kwenye viwango vya ubora wa Shirikisho la soka Ulaya (UEFA).

Arsenal bado ina nafasi ya kufuzu endapo kama itanyakua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, ambapo kwenye mchakato huo utazihusisha pia timu za Barcelona, Borussia Dortmund, RB Leipzig na Juventus, zinazosubiri tiketi kwa kupitia ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Timu nane za kwanza ambazo zimeshafuzu kucheza fainali hizo za Kombe la Dunia kwa timu za klabu mwaka 2025 zimeshafahamika, huku majina kibao ya timu kubwa yakikosa tiketi hiyo.

Timu 32 zitashiriki fainali hizo, ambapo timu mbili kutoka kila taifa itaruhusiwa kushiriki. Kutakuwa na timu 12 kutoka Ulaya, sita kutoka Amerika Kusini, nne kutoka kila upande, Asia na Afrika na Amerika, wakati moja itatoka huko Oceania na timu ya mwisho ni kutoka nchi mwenyeji, Marekani.

Michuano hiyo itachezwa kila baada ya miaka minne.

Liverpool na Man United hazitacheza fainali hizo mpya, licha ya kufahamika kama klabu kubwa kabisa England. Chelsea na Man City ni timu mbili za England zilizofuzu baada ya kushinda mataji ya Ligi ya Ma-bingwa Ulaya siku za karibuni. Chelsea ilishinda 2021 na Man City 2023, huku timu zilizopata tiketi ya moja kwa moja kushiriki fainali hizo ni zile zilizobeba ubingwa wa Ulaya kuanzia mwaka 2020.

Arsenal ina nafasi ya kukamatia tiketi endapo kama itanyakua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Arsenal imefanikiwa kutinga hatua ya mtoano ya 16 bora. Man United imepoteza fursa baada ya kukomea hatua ya makundi kwenye mikikimikiki hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, wakati Liverpool haikufuzu kabisa.

Real Madrid ilibeba ubingwa wa Ulaya ndani ya muda huo unaotakiwa, hivyo imefuzu michuano hiyo. Nafasi nyingine zilizobaki zitashindanisha timu zilizoshika nafasi za juu kipointi kwenye UEFA.

Kwenye kundi hilo kuna timu za PSG, Bayern Munich, Inter Milan, Porto na Benfica.

Barcelona, Borussia Dortmund, RB Leipzig, na Juventus nazo zitachuana kuwana nafasi kwa kupitia ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, tiketi ambayo inafukuziwa pia na Arsenal.

Mfumo wa sasa wa Klabu Bingwa Dunia zitakoma mwaka huu wa 2023. Man City itakwenda kuiwakili-sha Ulaya kwenye fainali hizo za dunia, ambapo itaanzia kwenye hatua ya nusu fainali kwa kumenyana na Urawa Reds.

Mtindo utakaotumika kwenye mfumo mpya wa Kombe la Dunia la timu za klabu ni uleule wa kama wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambapo timu zitapangwa kwenye makundi manane yenye timu nne kila moja. Timu mbili za juu kutoka kwenye kila kundi zitafuzu hatua ya mtoano.

Tofauti itakayojitokeza ni kwamba kwenye michuano hiyo itakapofika hatua ya mtoano, hakutakuwa na mechi mbili za nyumbani na ugenini, itapigwa mechi moja tu, ambayo itaamua ni timu gani itasonga raundi inayofuata.

Hakutakuwa na timu itakayoshindania mshindi wa tatu, kitu ambacho kitachochea michuano hiyo kuwa na upinzani mkali kwa sababu kila timu itahitaji ushindi ili kuvuna kitu.

Chanzo: Mwanaspoti