Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Ushrikiano na majadiliano ndio siri yetu"- Kocha Biashara

Biashara Vs Tripoli Mchezaji wa Al Ahly Tripoli akidhibitiwa na wanajeshi wa mpakani, Biashara United

Sat, 16 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya jana kuilaza Al Ahly Tripoli kutoka nchini Libya, kwa magoli 2-0, katika Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Kocha wa Biashara, Patrick Odhiambo, amefunguka baada ya mchezo kueleza hasa kilichopelekea kuibuka na ushindi huo.

Unajua sisi kabla ya mchezo huwa tunasikilizana, tunajadiliana na kutoa maamuzi kwa pamoja kama timu na sio maamuzi ya mtu mmoja mmoja"

Hivyo hata tunapokuwa uwanjani kila mtu anajua mimi ni nani, natakiwa nifanye nini na kwa wakati gani, na mwenzagu akichelewa mimi ni fanye kipi kwa kifupi ni ushirikiano wa hali ya juu" amesema kocha Odhiambo.

Biashara itasafiri kuwafata Al Ahly Tripoli kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa raundi ya kwanza kufuzu kwa hatua ya makundi kombe la Shirikisho, mchezo ambao utapigwa Oktoba 23.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live