Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ushirikina, ugomvi kikwazo Mashujaa FC

Abdallah Baresi Angalizo Bares aandika barua kuondoka Mashujaa

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye Kocha mkuu wa Mashujaa FC Abdallah Mohamed “BARESI” amefanya maamuzi ya kuandika barua ya kujiuzulu kuifundisha Timu hiyo iliyopanda Daraja msimu huu, ikitokea Ligi ya Championship.

Bares alikabidhiwa jukumu la kukinoa kikosi cha Mashujaa FGC, akichukuwa nafasi ya Kocha Meja Mstaafu Abdul Mingange, ambaye alifanya kazi kubwaya kuipandisha timu hiyo ya mkoani Kigoma kwa kuifunga Mbeya City katika hatua ya Play Off.

Imeelezwa kuwa Kocha Baresi amefanya maumuzi hayo kufuatia kuwepo kwa mpasuko (Migogoro) endelevu ya ndani ya timu baina viongozi, ikidaiwa baadhi yao wanahitaji imani za kishirikikina ziwe sehemu ya uendeshwaji wa klabu na wengine hawahitaji hizo imani.

Pili inadaiwa kuwa, kuna mpasuko baina ya wachezaji haswa wanaotoka Dar es salaam na mkoa wa Kigoma ambao ni wazawa, mambo ambayo yanapekelea Timu hiyo kushindwa kufanya vizuri katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kaze anukia Ihefu FC Hata hivyo bado haijathibitishwa na Uongozi wa Mashujaa FC kama wameafiki kujiuzulu kwa Kocha huyo ambaye ana uzoefu mkubwa katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara na ile ya Zanzibar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live