Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ushiriki wa Mamelodi kwenye African Football League mashakani

Mamelodi(1).png Ushiriki wa Mamelodi Sundowns kwenye African Football League mashakani

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zikiwa zimesalia wiki tatu kuanza kwa michuano ya Ligi ya Soka ya Afrika, Ushiriki wa Mamelodi Sundowns katika michuano hiyo upo shakani baada Bodi ya Ligi kuu Afrika Kusini (PSL) kuwataka Wabrazil hao wachague michuano hiyo au Ligi kutokana na Ushiriki wa Sundowns kutishia kuvuruga programu za Ligi na michuano mingine Nchini humo.

Sundowns watalazimika kusimamisha ratiba zake kwenye Ligi kwa muda mrefu jambo ambalo limelalamikiwa na vilabu Nchini humo kwa kuwa hatua hiyo itapelekea kuvuruga ratiba za msimu mzima ya Ligi kuu Nchini humo.

Bodi ya PSL inadai kuwa CAF ilichelewa kuwasilisha ripoti za Ushiriki wa Sundowns na kwamba taarifa hiyo ilikuja wakati ambapo tayari Ligi Kuu Nchini humo zimeanza.

Aidha ripoti zinaeleza kwamba mawasiliano ambayo Bodi ya Ligi walipokea kutoka Rwanda ambako ndio makao makuu ya African Football League hayakutoa maelezo ya kutosha kuhusu waandaaji wa michuano hiyo huku ikielezwa kuwa kumekuwa na mawasiliano hafifu kati ya CAF na Ligi Kuu Afrika Kusini juu ya michuano hiyo.

Sundowns ni miongoni mwa timu nane zilizochukuliwa kutoka Ligi zenye madaraja ya juu barani Afrika sambamba na mabingwa wa Afrika Al Ahly, Wydad Casablanca ya Morocco, Esperance, TP Mazembe, Enyimba ya Nigeria, Simba SC kutoka Tanzania, na Petro Atletico kutoka Angola.

Mashindano hayo mapya ya vilabu ambayo awali ilifahamika kama African Super League yataanza kutimua vumbi Oktoba 20, 2023, mwaka mmoja baada ya CAF kutangaza rasmi juu ya uwepo wa michuano hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live