Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ushindi wowote tunafuzu hata wa goli moja - Ahmed Ally

Ushindi Wowote Tunafuzu Hata Wa Goli Moja   Ahmed Ally Ushindi wowote tunafuzu hata wa goli moja - Ahmed Ally

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nafasi ya kufuzu kwa Simba ipo kwenye mikono yao na Meneja wa habari na mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally amesema faida waliyonayo ni kuwa na uwiano mzuri dhidi ya mpinzani wao anayewafuatia kwa ukaribu Wydad Casablanca kwani walipokutana Simba ilishinda magoli mengi zaidi.

“Utaratibu wa kufuzu umebadilika, sasa hivi CAF wanaangalia head to head yaani mlipokutana wenyewe kwa wenyewe matokeo yalikuwaje! Ikitokea sisi na Wydad tumelingana pointi itaangaliwa tulivyokutana.

“Wao walitufunga goli moja na sisi tuliwanyoa goli mbili Benjamin Mkapa maana yake tukiwafunga Jwaneng Galaxy tumefuzu moja kwa moja na sisi ni tofauti kwa sababu ushindi wowote ule tunafuzu hata goli moja”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live