Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ushindi sasa wampa kiburi kocha Biashara

4cc7dc1319648c4f8676ecf439f96a18 Ushindi sasa wampa kiburi kocha Biashara

Tue, 16 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA wa Biashara United, Francis Baraza amejitapa kuwa wamejipanga kuwazuia Simba wasichomoze na ushindi kwenye mchezo unaokuja wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Alhamisi ya wiki hii kwenye Uwanja wa Karume, mkoani Mara.

Simba imekuwa na wakati mzuri kila inapocheza kwenye ardhi ya Mara, kwani haijawahi kupoteza mchezo wa ligi hiyo tangu Biashara ilipopanda daraja.

Akizungumza juzi baada ya kikosi hicho kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC, Baraza alisema ameshafanya kikao na wachezaji wake na kuwataka kuwa na nidhamu kila wanapocheza kwenye uwanja wao huo ili kuhakikisha wanabakisha pointi zote.

“Simba ni timu nzuri na inawachezaji wazuri, lakini sioni sababu kama tunaweza kupoteza kwenye mchezo wetu unaokuja, nilifanya kikao nimewaambia wachezaji umuhimu wa kulinda ushindi kwenye michezo yetu iliyosalia.”

“Najua mchezo na Simba utakuwa mgumu kwakuwa hawajawahi kupoteza mchezo dhidi yetu lakini safari hii itawezekana nimewaambia wachezaji wangu nidhamu ya kuongeza umakini kulinda malengo yetu ya kutopoteza mchezo,” alisema.

Baraza alisema ushindi walioupa dhidi ya Mwadui umeongeza morali kwa wachezaji wake hivyo wanaenda kutumia siku zilizosalia kufanyia kazi kasoro zilizojitokeza kwenye mchezo uliopita.

“Tulipata shida kupata ushindi hadi dakika za nyongeza tulisawazisha na kuongeza bao na kutufanya kuondoka na pointi tatu, lakini dhidi ya Simba tutakuja na mfumo tofauti lolote linaweza kujitokeza ndani ya dakika 90,” alisema.

Biashara United inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza michezo 19, imeshinda michezo tisa, sare tano na kupoteza michezo mitano na inajipanga kucheza na Simba inaoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 39.

Chanzo: habarileo.co.tz