Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ushindi dhidi ya Dodoma Jiji wampa kiburi Pluijm

Hans Pluijm Sing.jpeg Kocha Mkuu wa Singida Big Stars Hans Van Pluijm

Wed, 29 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Singida Big Stars,Hans Van Pluijm amesema Dodoma Jiji imekuwa kipimo sahihi kuelekea mchezo wa Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) dhidi ya Mbeya City Aprili 2 mwaka huu katika Uwanja wa Liti mkoani Singida.

Juzi SBS ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Dodoma Jiji katika Uwanja wa Jamhuri mkoani hapa na kumalizika kwa wageni kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

SBS imeweka kambi Dodoma kujiandaa na mchezo wa Kombe la ASFC, dhidi ya Mbeya City huku Dodoma Jiji ikiajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union Aprili 13 mwaka huu.

Pluijm alisema Dodoma Jiji walikuwa bora kipindi cha kwanza huku wao wakicheza vizuri kipindi cha pili.

“Dodoma Jiji imecheza vizuri ni timu nzuri ingekuwa inacheza hivi kila siku naamini ingefika mbali na ingekuwa na pointi nyingi zaidi, mchezo dhidi ya Mbeya City utakuwa mgumu lakini kiafya na kiakili tupo tayari kwa mchezo huo,” alisema kocha huyo.

Kipa wa timu hiyo, Benedict Haule alisema makosa yaliyojitokeza katika mchezo huo wa kirafiki anaamini benchi la ufundi watayafanyia kazi kabla ya mchezo dhidi ya Mbeya City.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live