Mchambuzi wa masuala ya kandanda hapa nchini Tanzania akizungumzia hali ya usajili katika kikosi cha klabu ya simba Alex Ngereza amesema kwamba, klabu ya Simba imeajili wachezaji wa viwango vya chini ambao hawataweza kuisaidia timu hiyo kuvuka robo fainali ya CAF.
Ngereza amesema hayo kufuatia usajili walioufanya Simba Sc mpaka sasa huku kukiwa na kazi kubwa kwa Mnyama kuhakikisha anavuka robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo amekuwa akikomea hatua hiyo hiyo kwa takribani miaka mitano.
"Ukiangalia vilabu 10 bora vya Afrika ambavyo Simba nayo ipo, sajili zinazofanyika ni tofauti na sajili wanazozifanya Simba.
"Wachezaji ambao wanawasajili sio 'level' za wachezaji ambao wanasajiliwa na vilabu vingine vikubwa vya Afrika, wanaweza kufika hatua ya robo fainali lakini hawawezi kuvuka hatua ya nusu fainali," amesema Ngereza.
Mpaka sasa Simba imesajili wachezaji wafuatao, Luis Jefferson, Duchu Kameta, Malone, Hussein Kazi, Abdullah Hamis, Luis Miquissone, Fabrice Ngoma, Aubin Kramo, Willy Onana Wengine, Shabani Chilunda.
Walioachwa ni Beno Kakolanya, Mohammed Ouatara, Ismail Sawadogo, Joash Onyango, Augustine Okrah, Nelson Okwa, Victor Akpan, Gadiel Michael, Jonas Mkude, Pape Sakho na Habibu Kyombo.