Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usajili wa straika mpya Simba ni pigo

Jobe Simba SC Omar Jobe

Tue, 16 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usajili wa Mgambia Omar Jobe uliofanywa na Simba leo ni kama umeipa pigo timu aliyotoka ya Zhenis Astana ya Kazakhstan.

Uwezo ulioonyeshwa na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 katika kufumania nyavu hapana shaka unaipa kazi ngumu Zhenis kusaka mbadala wake.

Takwimu za mitandao mbalimbali, zinaonyesha kuwa Jobe katika  mechi 25 alizoichezea Zhenis Astana kabla ya kujiunga na Simba, alikuwa ameifungia mabao 13 katika mechi 25.

Kabla ya hapo, mshambuliaji huyo anayetumia zaidi mguu wa kulia, alikuwa ametoka kuifungia Sheikh Jamal Dhanmondi ya Bangladesh mabao 25 katika mechi 32.

Makali ya Jobe hayapo katika kufunga mabao tu bali pia hata kupiga pasi za mwisho na ushahidi wa hilo ni takwimu zake za misimu miwili iliyopita.

Akiwa na Dhanmondi alipiga pasi tano za mwisho na alifanya hivyo mara katika kikosi cha Zhenis.

Hiyo inamfanya Jobe kuhusika na mabao 18 katika mechi 25 za Zhenis na amehusika na mabao 30 katika mechi 32 za Dhanmondi ya Bangladesh.

Hata hivyo mshambuliaji huyo anaonekana amekuwa na tabia ya kutodumu kwenye timu kwani katika miaka miwili amezichezea timu tano. Timu hizo ni Struga, Shkendija, Neman Grodno, FC Zhenis na Dhanmondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live