Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usajili wa mastaa Ulaya unaoweza kufanyika mwezi Januari

Manchester United Wambembeleza De Gea Kurejea Old Trafford David De Gea

Sat, 9 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kutokana na vikosi vingi kukumbwa na wachezaji wenye majeraha, makocha wamelalamika na sasa tetesi za usajili zimeibuka, kuna uwezekano baadhi ya klabu zikafanya usajili katika dirisha dogo la Januari ili kuboresha vikosi vyao.

Timu kama Manchester United, Newcastle, Tottenham, Chelsea, Real Madrid, Barcelona zimekumbwa na wachezaji wengi wenye majeraha msimu huu, hivyo zinaweza kuboresha vikosi vyao kwa kufanya usajili.

Kwa sasa macho ya mashabiki yataelekea katika usajili wa dirisha dogo, ambalo litafunguliwa Januari mwakani, kwani klabu zitawekeza pesa kusaka wachezaji wanaowahitaji.

Ingawa usajili wa dirisha dogo haupewi sana kipaumbele tofauti na usajili wa kiangazi, kwa sababu ni vigumu kupata wachezaji sahihi wanaotakiwa na makocha.

Wakati tunaelekea katika dirisha dogo la usajili, uhamisho wa wachezaji hawa unaweza kutokea Januari.

David de Gea (Hana timu)

De Gea amezikataa ofa kutoka Saudi Arabia na Marekani huku akitoa muda wa kuchagua timu ambayo atajiunga nayo. Kipa huyo wa zamani wa Manchester United yupo huru tangu alipoondoka baada ya miaka 12, taarifa zimeripoti huenda akajiunga na Newcastle akazibe pengo la Nick Pope aliyeumia kwenye mechi ya Ligi Kuu England ilipomenyana na Manchester United.

Denzel Dumfries- Inter Milan

Dumfries alikiwasha Inter Milan msimu uliopita na alipambana sana katika fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City. kwa mujibu wa Calciomercat, Manchester United, Chelsea na Tottenham zinawania saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi mwenye thamani ya Pauni 43.5 milioni. Wakati huohuo, Spurs ilijiandaa kumtoa Emerson kama sehemu ya makubaliano ya kumpata Dumfries.

Jean-Clair Todibo- Nice

Beki wa kimataifa wa Ufaransa anayetajwa sana kuwa Janauri anaweza kuondoka Nice inayomilikiwa na Sir Jim Ratcliffe. Kocha Erik ten Hag anamfukuzia beki huyo na kuna uwezekano akasamjili ili aboreshe safu yake ya ulinzi. Wakati huohuo, Spurs na Liverpool zimehusishwa na beki huyo mwenye umri wa miaka 23.

Antonio Silva- Benfica

Beki huyo ni tegemeo Benfica licha ya kuwa na umri wa miaka 20 na amekuwa na mchango mkubwa sana. Aidha uhamisho wa beki huyo unaweza kuwa ghali kwani katika kipengele cha mkataba wake amewekewa kifungu cha Pauni 85 milioni hivyo timu inayomuhitaji ijipange.

Alphonso Davies- Bayern Munich

Beki wa kimataifa Canada anawindwa vikali na Real Madrid ambayo imepanga kumsajili dirisha la usajili la kiangazi Julai mwakani. Hata hivyo, Bayern imepanga kumwongeza mkataba mpya kipindi cha Januari ili kuitibulia Los Blancos. Kwa mujibu wa Bild kutoka Ujerumani, Liverpool na Manchester City zimeonyesha kuvutiwa na beki huyo mwenye kasi.

Jota - Al-Ittihad

Nyota wa kimataifa wa Ureno anapitia kipindi kigumu tangu alipotua Al-Ittihad ya Saudi Arabia, kuna wezekano akaondoka Januari akasake maisha sehemu nyingine baada ya kumshindwa kung’ara. Winga huyo wa zamani wa Celtic anatamani aungane na kocha wake Ange Postecoglou anayeinoa Tottenham.

Douglas Luiz - Aston Villa

Kwa muda mrefu Arsenal imevutiwa na kiungo wa Aston Villa, Douglas Luiz lakini uhamisho wake ukashindikana. Kocha Mikel Arteta anapanga kumsajili amchezeshe pamoja na Declan Rice walete ubunifu kwenye kiungo.

Pedro Neto- Wolves

Mreno huyo amekuwa hatari msimu huu kwani amefunga bao moja na asisti nane katika michezo 10 ya Ligi Kuu England. Arsenal imemfuatilia na itaangalia uwezekano wa kumsajili Januari akaongeze nguvu katika mbio za kuwania ubingwa msimu huu.

Ivan Toney- Brentford

Adhabu yake ya kufungiwa baada ya kugundulika alikuwa akicheza kamari itamalizika Januari 17 na huenda akaondoka Brentford, huku Arsenal ikihusishwa. Klabu za Ligi Kuu England zilishindwa kumsajili fowadi huyo mwenye thamani ya Pauni 100 milioni usajili uliopita.

Victor Osimhen-Napoli

Straika huyo alikuwa mfungaji bora wa Serie A msimu uliopita akicheka na nyavu mara 26 huku akiisaidia Napoli kubeba ubingwa wa ligi. Chelsea inajiandaa kuvunja rekodi ya usajili ya Pauni 115 milioni iliyoitoa kwa ajili ya kiungo wa zamani wa Brighton, Moises Caicedo aliyejiunga nayo kwenye usajili uliopita.

Chanzo: Mwanaspoti