Msemaji wa zamani wa Yanga Haji Manara ameeleza kushangazwa na uamuzi wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) kuzuia usajili wa winga Tuisila Kisinda kujiunga na Yanga akitokea klabu ya RS Berkane.
Manara amesema Yanga imekamilisha usajili wa Kisinda kabla ya dirisha la usajili kufungwa, wamewasilisha majina ya wachezaji 12 wa kigeni waliosajiliwa ndani ya wakati lakini wanashangaa kwa nini Kisinda azuiwe ikiwa hata ITC yake anayo?
"Kumzuia Tuisila kisinda kucheza Yanga Kwa sababu zisizokidhi masharti ya kanuni ni mwendelezo wa uonevu dhidi yetu. Kosa lipo wapi wakati usajili wake umewahi kabla dirisha halijafungwa? Mwisho lini Club kupangiwa muda wa kuwasilisha majina ya usajili? Iwe Kwa Wachezaji local au foreigners?"
"Kamati inayohusika na Hadhi za Wachezaji imekaa lini hadi Katibu utoe hukumu? Tunafanya hivi vitu kumfurahisha nani? Kwa Interest ya kina nani?," alihoji Manara.
Taarifa:
Wananchi, TFF bila sababu zenye mashiko, imezuia usajili wa winga wetu Tuisila Kisinda kusajiliwa Yanga, ilhali tumewahi deadline ya mwisho ya kabla dirisha la usajili kufungwa.
Klabu imewasilisha majina ya wachezaji 12 wa kigeni watakaocheza msimu ujao, jina la Tuisila likiwemo kabla dirisha halijafungwa, why katibu ujipe jukumu la kamati ya hadhi za wachezaji na kuandika barua ya maamuzi?
Kwa nini usisubiri maamuzi ya Kamati? Uharaka wa nn? Hiki kiburi kimetokea wapi?
Mnajisikiaje kila siku kuifanyia hivi Yanga? ITC anayo, kawahi deadline, why mnatutendea hivi? Yanga imekuwa mnyonge nchi hii? No No No No, imezidi sasa, kwa ilivyo, ndio Tuisila hachezi hvyo na hatuna la kufanya, Mamlaka ishaamua,” amesema Manara.