Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usajili wa Sandro Tonali Newcastle waweka rekodi

Sandro Tonali Usajili wa Sandro Tonali Newcastle waweka rekodi

Mon, 3 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Newcastle United ya Ligi Kuu England EPL imekamalisha usajili wa kiungo Sandro Tonali kutoka AC Milan ya Italia kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 60 zaidi ya Bilioni 183.999 za Kitanzania.

Tonali raia wa Italia ana umri wa miaka 23 amesaini mkataba wa miaka 5 kujiunga na Newcastle United ambapo ataendelea kuwa klabuni hapo hadi mwaka 2028.

Tonali ameweka rekodi kuwa mchezaji ghali zaidi aliyenujuliwa na Newcastle akivunja rekodi ya Alexander Isak ambaye alijiunga na Newcastle kwa dau la Pauni milioni 55 akitokea Real Sociedad.

Tonali aliisaidia Milan kutwaa taji lake la kwanza la Serie A katika kipindi cha miaka 11 msimu wa 2021-22 na alikuwa mtu muhimu katika harakati zake za nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.

“Kwanza kabisa, nataka kuwashukuru Newcastle United kwa sababu inanipa nafasi kubwa katika maisha yangu ya soka,” Tonali alisema. “Nataka kulipa uaminifu uwanjani, nikitoa yote yangu, kama ninavyofanya siku zote.”

Ada hiyo itamfanya Tonali kuwa mchezaji ghali zaidi wa Kiitaliano wa wakati wote huku pia ikiwa ni rekodi ya kuuzwa kwa AC Milan, ikipata euro milioni 68 ambazo Real Madrid walilipa kwa kiungo wa Brazil Kaka mnamo 2009.

Huu ni usajili wa kwanza kwa Newcastle United kwenye dirisha hili kubwa la usajili kuelekea msimu ujao wa 2023-24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live