Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usajili wa Mykhailo Mudryk Chelsea wapigwa zengwe

Mykhailo Mudryk Criticism Mykhailo Mudryk

Sat, 25 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gwiji wa Arsenal, Paul Merson amekosoa usajili wa Pauni 600 milioni uliofanywa na Chelsea, huku akipigilia nyundo uhamisho wa Mykhailo Mudryk kwamba hana anachokifanya huku akimtaja Noni Madueke kuwa hana uwezo.

Mmiliki wa Chelsea, Todd Boehly ametumia Pauni 326 milioni kwenye dirisha la usajili la Januari mwaka huu, ikiwa ni zaidi ya theluthi moja ya usajili wote uliofanywa kwenye Ligi Kuu England, ambao umegharimu Pauni 815 milioni.

Kwenye dirisha hilo la Januari, Chelsea ilimsajili Mudryk kwa Pauni 97 milioni, huku ikilipa Pauni 107 milioni kunasa huduma ya kiungo Enzo Fernandez. Kuna wachezaji nane walisajiliwa na The Blues kwenye dirisha hilo la Januari, akiwamo Benoit Badiashile na winga Madueke, aliyesajiliwa kwa Pauni 35 milioni kutoka PSV.

Lakini, kichapo cha Jumamosi iliyopita kutoka kwa Southampton kilikuwa na maana kwamba timu hiyo imepata ushindi kwenye mechi mbili tu kati ya 14 za kwenye Ligi Kuu England chini ya Graham Potter.

Mudryk alionyesha uhai kwenye mechi ya kwanza Chelsea iliyomalizika kwa sare ya bila kufungana dhidi ya Liverpool mwezi uliopita, lakini tangu wakati huo hajafunga wala kuasisti.

Na Merson anaona Chelsea wamepigwa, akisema: “Watu wanadhani Potter si mtu sahihi kwenye benchi la Chelsea, lakini nadhani kwa upande wangu, anapaswa kupewa muda. Ona, mchezaji kama Mykhailo Mudryk, wamemsajili kwa pesa nyingi, lakini hakuna anachokionyesha. Huwezi kumpa muda mchezaji ambaye umemsajili kwa pesa nyingi kiasi kile. Na huyu Noni Madueke ni bora hata ya Raheem Sterling na Christian Pulisic.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live