Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usajili wa Kibu hatukulala wiki mbili - Simba

Kibu  Simba Kauli Usajili wa Kibu hatukulala wiki mbili - Simba

Wed, 24 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa hakuna usajili ambao uliwatetesa viongozi hao kama ule wa kiungo mshambuliaji wao, Kibu Denis.

Kauli hiyo ya Ahmed imekuja ikiwa ni siku chache baada ya mchezaji huyo kugoma kujiunga na kambi ya klabu huko Misri na kutimkia nchini Norway ambako anadaiwa kupata dili.

"Hakuna usajili uliotutesa Simba kama wa kumuongezea mkataba Kibu Denis. Alikuwa anasema ntaongeza mkataba, ntaongeza mkataba Anapitia huku anatokea huku. Wavimba macho nao walikuwa wanamvizia Hatukulala wiki mbili.

"Watu wanasema ana goli moja. Ndio ana goli moja lakini anajituma sana. Kibu ni aina ya wachezaji ambao wanacheza kama timu za baba zao, Hakuna timu inatamani kukutana na Kibu," amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live