Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usajili wa Hussein Kazi waanza kulipa Simba

Hussein Kazi Usajili wa Hussein Kazi waanza kulipa Simba

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matarajio ya Klabu ya Simba kwa kitasa Hussein Kazi hakika yameanza kulipa baada ya mchezaji huyo kuanza kuonyesha uwezo mkubwa alio nao.

Simba ilimsajili Kazi, Julai 20, 2023 ili kuimarisha safu yao ya ulinzi, na jana imewalipa katika hatua ya nusu fainali kwa kuziba nafasi ya mkongwe Kennedy Juma katika mabadiliko ya kimchezo.

"Hussein (23) ni kijana mwenye uwezo mkubwa na tunatarajia atakuwa ingizo bora kikosini," nukuu ya Simba katika utambulisho wa Kazi.

"Katika eneo la mlinzi wa kati, Hussein ataungana na wazoefu Henock Inonga, Kennedy Juma na Che Fondoh Malone," Imeeleza taarifa hiyo ya Julai 20, 2023.

Kazi ni zao la Shule ya Sekondari Azania 'Azaboi' iliyopo Upanga, Dar es Salaam, kuanzia 2010-2013 chini ya Mwalimu Mkuu Ngozye.

Hussein amecheza soka la kulipwa nchini Shelisheli katika timu ya Forester FC kabla ya kujiunga na Mbeya Kwanza, Polisi Tanzania na Geita Gold.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live